26
Sun, Jan
4 New Articles

Marcelline Awataka Watumishi Kufanya Kazi kwa Usahihi

News
Typography

 Mkurugenzi wa Utawala, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Bw. Benard P. Marcelline, amewataka watumishi kutumia mafunzo wanayoyapata katika kufanya kazi za tume kwa uhakika na usahihi zaidi.

 

Marcelline aliyasema hayo alipokuwa akitoa ufafanuzi kwenye semina, iliyohusisha maafisa wa Tume na wadau wengine  kuhusu kutatua na kushughulikia malalamiko yanayohusu vurugu za kimsimamo na kiitikadi (Violent Extremism)

Semina hiyo, ililenga kuwajengea uwezo watumishi ili kutolea taarifa masuala yote yanayohusu vurugu za kimsimamo kwa ngazi zote ili kulinda usalaama kwa nchi yetu.

Vilevile yalilenga kuwajulisha watumishi njia sahihi ya kutoa taarifa pamoja na kupanua wigo wa maafisa katika kutoa taarifa hizo.

Akitoa mafunzo, mwezeshaji wa semina hiyo Bw. Othman Salum, alizitaja njia sahihi zinazoweza kutumiwa na tume ili kuzuia vurugu nchini kuwa ni pamoja na; Kuendelea kutoa elimu inayohusu misingi ya utawala bora nchini, uboreshaji na ukuaji wa uchumi, kuwepo kwa ushawishi na utetezi wa serikali juu ya mambo gandamizi, maboresho katika jeshi la polisi, elimu ya kujitegemea pamoja na kufanya tafiti mbalimbali zinazohusisha masuala ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

Semina hiyo ilianza Juni, 21 - 22 2018, Makao makuu THBUB. Jijini Dar Es Salaam, na kuhudhuliwa na watumishi wa Tume kutoka Dar Es Salaam na Ofisi za matawi; Pemba, Unguja, Lindi na Mwanza.