08
Sat, Aug
3 New Articles

Muya ahudhuria mkutano mkuu AOMA

Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Hajjat Fatuma Muya( wa pili kutoka kushoto) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mheshimiwa Ernest Mangu ( wa pili kutoka kulia) walipokutana jijini Kigali, Rwanda. Wengine ni wajumbe waliohudhuria Mkutano mkuu wa AOMA.

News
Typography

 

Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Hajjat Fatuma Muya amehudhuria mkutano mkuu wa  sita (6) wa  mwaka wa Tume za Uchunguzi za Afrika (AOMA).

Mkutano huo uliohusisha takribani wawakilishi arobaini na sita (46) kutoka  tume za uchunguzi za Afrika  ulifanyika katika hoteli ya Marriot iliyopo jijini Kigali, Rwanda Novemba 27- 30, 2018 .

 

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mtendaji huyo, Mkutano huo  wa mwaka ulikuwa na lengo la kufanya uchaguzi wa viongozi wa  umoja wa tume hizo za uchunguzi za Afrika (AOMA).

Muya  aliongeza kwa kusema kuwa   wajumbe wa mkutano huo walitumia nafasi hiyo kupitisha baadhi ya marekebisho ya katiba ya umoja huo na  mpango mkakati wa miaka mitatu (3) wa taasisi hiyo.

Katika mkutano huo, Muya aliongozana na Afisa Uchunguzi  Mkuu, Vicent Mbombo.

Umoja wa tume za uchunguzi za Afrika (AOMA) umekuwepo tangu mwaka 1990 kwa lengo la kutia chachu maendeleo ya taasisi hizo za kichunguzi ili kuboresha utawala bora, utawala wa sheria na haki za binadamu barani Afrika.