23
Sun, Feb
12 New Articles

THBUB Yafanya Mazungumzo na Shirika la CEFA

News
Typography

Na Getrude Alex

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), hivi karibuni ilifanya kikao kazi na mwakilishi wa Asasi ya Kiraia ijulikanayo kwa jina la “CEFA” (Comitato Europeo per la Formazione el’ Agricoltura Onlus)  

Mazungumzo hayo ya siku moja yalilenga kujenga mashirikiano ya kikazi, baina ya THBUB na shirika la CEFA hususani kwenye suala la kukomesha ukatiri  na mauaji kwa  watoto na watu wenye ulemavu wa Ngozi.

 

 

Akizungumzia suala hilo, mwakilishi wa CEFA Bw. Gabriele Maneo, Alisema mradi huo waliokusudia kufanya na Tume utachukua takribani miaka miwili (2) kukamilika, ambapo shirika hilo linategemea kudhamini gharama za mradi kwa kiasi kikubwa endapo watafanikisha kupata ufadhiri kwa wakati.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji wa Tume Bw. Fransis Nzuki, alimweleza Bw. Gabriel kuwa, Tume imekuwa na mashirikiano mazuri na wadau mbalimbali wa haki za binadamu, na kuahidi kushirikiana vyema na shirika la CEFA  huku  wakizingatia kanuni na sheria za Tume.

Kikao hicho kilichofanyika Mei 3, 2019, kilihudhuriwa na wajumbe wapatao  kumi na saba (17) kutoka THBUB na mwakilishi (1) kutoka CEFA.