24
Thu, Sep
0 New Articles

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) tumepokea kwa majonzi makubwa taarifa ya kifo cha ghafla cha mpendwa wetu, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa, kilichotokea usiku wa kuamkia leo Julai 24, 2020 huko jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mfupi.Soma zaidi

Pongezi kwa Mhe.John Pombe Magufuli kwa Tanzania kuingia Katika Orodha ya Nchiza Uchumi wa Kati.

Julai 1, 2020 Benki ya Dunia iliutangazia ulimwengu Kuwa imeirodhesha Tanzania katika orodha ya nchi za uchumi wa Kipato cha kati, hatua iliyojiri miaka mitano kabla ya muda uliopangwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2025. Soma zaidi

Tamko la THBUB Wakati wa Siku ya Kupinga Ajira kwa Watoto Juni 12 ,2020

Tarehe 12 Juni ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ajira kwa Mtoto Duniani -World Day against Child Labour .Siku ilianzishwa na Shirika la Kazi Duniani(ILO)MWAKA 2002 kwa madhumuni ya kutoa elimu na kufanya uchechemuzi ili kuzuia utumikishwaji kwa watoto.Soma zadi

TAMKO LA THBUB KUMPONGEZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KWA HOTUBA YA KULIFUNGA BUNGE LA 11 ALIYOITOA KATIKA UKUMBI WA BUNGE, DODOMA TAREHE 16 JUNI, 2020

Tarehe 16 Juni 2020, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa Hotuba ya Kufunga Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ukumbi wa Bunge, Dodoma. Turne ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora (THBUB) inatoa pongezi za dhati kwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Hotuba yake iliyojaa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano cha uongozi wake, yaani kuanzia mwaka 2015 hadi 2020. Soma zaidi

Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Juni 5, 2020

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana na Watanzania wote katika kuadhimisha Siku ya Mazingira duniani ambayo kilele chake ni Juni 5, 2020. 

Kama Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Kitaifa Mwaka huu inavyosema Tuhifadhi Mazingira: Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi, hivyo, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nayo kupitia Maadhimisho haya inapenda kuwakumbusha Wananchi wajibu wao wa kutunza na kuhifadhi mazingira kwa sababu ustawi wa viumbe hai akiwemo binadamu unategemea mazingira mazuri.Soma zaidi

 

Tamko la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Juni 16, 2020

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana na wadau wote wa haki za watoto katika kuadhimisha “Siku ya mtoto wa Afrika”. Siku hii inaikumbusha dunia juu ya mauaji ya watoto wapatao 2,000 wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini, waliouawa kikatili miaka 44 iliyopita na iliyokuwa Serikali ya Makaburu.Soma zaidi

Tamko la THBUB wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kukuza Uelewa wa Dhuluma dhidi ya Wazee Duniani,juni 15,2020

Juni 15 kila mwaka Tanzania na jumuiya ya kimataifa huadhimisha Siku ya "Kukuza Uelewa dhidi ya Wazee Duniani (world Elder Abuse Awareness Day. " Lengo la siku hii iliyopitishwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Azimio Na.A/RES/66/127 LA Desemba 19,2011 ni kutoa fursa kwa jamii kukuza uelewa wa dhulma na unyanyasaji wanaokumbana nao wazee duniani kote na kupambana na tatizo hilo.Soma zaidi

Kupongeza juhudi za Serikali dhidi ya Mapambano ya Mlipuko wa Maradhi yanayosababishwa na virusi vya Corona

Itakumbukwa kuwa katikati ya mwezi Machi mwaka huu Serikali ilitangaza mapambano rasmi dhidi ya maradhi yanayosababishwa na virusi vya Corona ambavyo hivi karibuni imekuwa ni janga kubwa duniani.Soma zaidi

 

Tamko la THBUB wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kuongeza uelewa KUHUSU Ualbino,Juni 13,2020

LEO juni 13,2020 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)inaungana na wadau wote wa haki za watu wenye Ualbino duniani katika kuadhimisha  Siku ya Kimataifa ya Kuongeza Uelewa Kuhusu Ualbino "

- International Albinism Awareness  Day”  ikiwa na Kauli mbiu “Haki sawa kwa Wote: Boresha Afya ,Elimu na Ajira kwa Watu wenye Ualbino."Soma zadi

Ujumbe wa THBUB Siku ya Maji, Machi 22, 2020

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana  na Watanzania wote katika kuadhimisha Siku ya Maji Duniani ambayo leo Machi 22, 2020 ndio kilele chake.

Tume inatambua kuwa  haki ya maji ni miongoni mwa haki za kijamii  kama ilivyo haki nyingine, hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa watanzania wanaendelea kufurahia haki hiyo kwa uhakika.

More Articles ...

Page 1 of 3
Sign up via our free email subscription service to receive notifications when new information is available.