14
Tue, Jul
7 New Articles

Pongezi kwa Mhe.John Pombe Magufuli kwa Tanzania kuingia Katika Orodha ya Nchiza Uchumi wa Kati.

Julai 1, 2020 Benki ya Dunia iliutangazia ulimwengu Kuwa imeirodhesha Tanzania katika orodha ya nchi za uchumi wa Kipato cha kati, hatua iliyojiri miaka mitano kabla ya muda uliopangwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2025. Soma zaidi

TAMKO LA THBUB KUMPONGEZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KWA HOTUBA YA KULIFUNGA BUNGE LA 11 ALIYOITOA KATIKA UKUMBI WA BUNGE, DODOMA TAREHE 16 JUNI, 2020

Tarehe 16 Juni 2020, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa Hotuba ya Kufunga Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ukumbi wa Bunge, Dodoma. Turne ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora (THBUB) inatoa pongezi za dhati kwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Hotuba yake iliyojaa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano cha uongozi wake, yaani kuanzia mwaka 2015 hadi 2020. Soma zaidi

Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Juni 5, 2020

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana na Watanzania wote katika kuadhimisha Siku ya Mazingira duniani ambayo kilele chake ni Juni 5, 2020. 

Kama Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Kitaifa Mwaka huu inavyosema Tuhifadhi Mazingira: Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi, hivyo, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nayo kupitia Maadhimisho haya inapenda kuwakumbusha Wananchi wajibu wao wa kutunza na kuhifadhi mazingira kwa sababu ustawi wa viumbe hai akiwemo binadamu unategemea mazingira mazuri.Soma zaidi

 

Tamko la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Juni 16, 2020

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana na wadau wote wa haki za watoto katika kuadhimisha “Siku ya mtoto wa Afrika”. Siku hii inaikumbusha dunia juu ya mauaji ya watoto wapatao 2,000 wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini, waliouawa kikatili miaka 44 iliyopita na iliyokuwa Serikali ya Makaburu.Soma zaidi

Mwenyekiti wa THBUB, Jaji (Mst) Mathew Mwaimu (kulia) akiongea na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma, Jaji (Mst) Harold Nsekela (Kushoto) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma jana. Lengo la ziara hiyo ya THBUB ni kuimarisha ushirikiano na Sekretarieti ya Maadili

Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma, Jaji (Mst) Harold Nsekela amezishauri taasisi zinazosimamia utawala bora kushirikiana kwa karibu ili waweze kutekeleza majukumu yao vizuri. 

Jaji Nsekela alitoa rai hiyo katika ofisi yake jijini Dodoma jana alipokutana na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji (Mst) Mathew Mwaimu.

Tamko la THBUB wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kukuza Uelewa wa Dhuluma dhidi ya Wazee Duniani,juni 15,2020

Juni 15 kila mwaka Tanzania na jumuiya ya kimataifa huadhimisha Siku ya "Kukuza Uelewa dhidi ya Wazee Duniani (world Elder Abuse Awareness Day. " Lengo la siku hii iliyopitishwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Azimio Na.A/RES/66/127 LA Desemba 19,2011 ni kutoa fursa kwa jamii kukuza uelewa wa dhulma na unyanyasaji wanaokumbana nao wazee duniani kote na kupambana na tatizo hilo.Soma zaidi

Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tulia Ackson (kushoto) akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Mohamed Khamis cheti cha kutambua mchango wa Tume katika kuwawezesha Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kutimiza majukumu yao. Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wauguzi Duniani yalifanyika hospitalini hapo jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. (Mei 15, 2020).

Tamko la THBUB wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kuongeza uelewa KUHUSU Ualbino,Juni 13,2020

LEO juni 13,2020 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)inaungana na wadau wote wa haki za watu wenye Ualbino duniani katika kuadhimisha  Siku ya Kimataifa ya Kuongeza Uelewa Kuhusu Ualbino "

- International Albinism Awareness  Day”  ikiwa na Kauli mbiu “Haki sawa kwa Wote: Boresha Afya ,Elimu na Ajira kwa Watu wenye Ualbino."Soma zadi

 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa na Taarifa ya vitendo vinavyofanywa na baadhi ya  Madaktari ana Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Mwananyamala vya kuwanyanyapaa na kuwasubua wagonjwa hao kwenda kufanya vipimo vya Korona kabla ya kuanza kupata matibabu.Soma zaidi

Tamko la THBUB Wakati wa Siku ya Kupinga Ajira kwa Watoto Juni 12 ,2020

Tarehe 12 Juni ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ajira kwa Mtoto Duniani -World Day against Child Labour .Siku ilianzishwa na Shirika la Kazi Duniani(ILO)MWAKA 2002 kwa madhumuni ya kutoa elimu na kufanya uchechemuzi ili kuzuia utumikishwaji kwa watoto.Soma zadi

Salamu za Pole kwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepokea kwa mshituko mkubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga (Mb) kilichotokea leo alfajiri Mei 01, 2020 Jijini Dodoma.

Tume inatoa pole kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuondokewa na kiongozi  mchapakazi, mwadilifu, mzalendo na mwanadiplomasia mahiri aliyeiwakilisha na kuipigania Tanzania katika nyanja za Kimataifa kwa miaka mingi.Soma zaidi

More Articles ...

Sign up via our free email subscription service to receive notifications when new information is available.