23
Sat, Jan
1 New Articles

Mwakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Josephine Lyengi akitoa mada katika kikao kazi cha kujadili hali halisi ya haki za binadamu nchini na kuibua matukio ambayo bado yanaonekana ni changamoto kubwa na kuyatengenezea mpango kazi wa kushughulikia. Kikao hicho kinafanyika Mkoani Morogoro kuanzia Oktoba 24—25, 2019.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imekutanisha makundi ya haki za binadamu iliyoyaunda ili kujadili hali ya haki za binadamu na kuibua matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu kwenye makundi ya wanawake, watoto na watu wenye ulemavu ili kuandalia mpango kazi wa kwenda kuyashughulikia.

Wakili Clarence Kipobota akisisitiza jambo katika kikao kazi cha siku tatu cha kupeana mrejesho wa kazi walizofanya kati ya Tume na AZAKI na kuandaa taarifa ya pamoja ya robo mwaka ya hali ya haki za binadamu nchini kilichofanyika Mkoani Morogoro, Oktoba 21—23, 2019.

Asasi za Kiraia (AZAKI) zimeshauriwa kuitumia Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kufikisha taarifa kwa jamii kwani ndio taasisi pekee ya kitaifa iliyokasimiwa mamlaka ya kulinda, kuhifadhi, kutetea na kuhamasisha haki za binadamu nchini.

Bi.Madenge afungua mafunzo ya Watendaji wa Kata kuhusu haki za Binadamu,yaliyofanyika katika mkoa wa Lindi Julai 8, 2019.

Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Rehema Madenge amewataka Watendaji wa kata katika wilaya za Mkoa wa Lindi kusimamia haki za binadamu na upatikanaji wa haki kisheria.

Madenge alitoa wito huo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa watendaji wa kata kuhusu haki za binadamu na upatikanaji haki kisheria yaliyofanyika katika mkoa wa Lindi Julai 8, 2019.

Kaimu Katibu Mtendaji, Hajjat Fatuma Muya (katikati) akiongea katika warsha ya kupeana mrejesho wa kazi za robo mwaka (Julai-Septemba) iliyofanyika kwa siku tatu (3), kuanzia Oktoba 21—23, 2019 Mkoani Morogoro. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Elimu kwa Umma, Mawasiliano, Utafiti na Nyaraka kutoka Tume, Alexander Hassan, na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi kitengo cha Mipango kutoka Tume, Laurent Burilo.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia (AZAKI) washirika wamekutana  Mkoani Morogoro kuandaa taarifa ya pamoja ya robo mwaka ya kuanzia mwezi Julai hadi Septemba, 2019 ya hali ya haki za binadamu nchini.

THBUB yakutana na Wadau kubuni mbinu za kuelimisha jamii

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kuwashirikisha wadau wake kutoka taasisi za Serikali, Asasi za Kiraia na Vyombo vya habari wamekutana katika kikao kazi cha kubuni mbinu mbalimbali zinazolenga kuongeza uelewa kuhusu haki na haki za binadamu, hususan haki za wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.

Afisa wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mbaraka Kambona (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi ya SIFO alipoitembelea taasisi hiyo Septemba 26, 2019. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa SIFO, Juma Issa Ngaona, wa pili kutoka kushoto ni Afisa Programu wa SIFO, Kissonga Mario na wa pili kutoka kulia ni Katibu wa SIFO, Hashim Mohamed.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) hivi karibuni ilifanya ziara ya kutembelea Asasi za Kiraia ishirini (20) ambazo iliingia nazo mkataba wa ushirikiano zilizopo katika mikoa ya Tanzania bara na visiwani.

Mratibu wa Mradi wa upatikanaji wa haki, Laurent Burilo akitoa mada kwa ufupi kuhusu mradi wa upatiakanaji wa haki katika kikao kazi cha kuandaa hadidu za rejea na muongozo kwa ajili ya makundi ya utetezi wa haki za binadamu kinachofanyika mkoani Morogoro kuanzia Juni 20-22, 2019.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kushirikiana na wadau wake wanaandaa hadidu za rejea na muongozo kwa ajili ya kuyawezesha makundi ya utetezi wa haki za binadamu kufanya kazi zake vizuri.

Akifungua kikao kazi cha kuandaa hadidu za rejea na muongozo kwa ajili ya makundi hayo ya haki za binadamu kinachofanyika mkoani Morogoro kuanzia Juni 20-22, 2019,   Mkurugenzi wa Idara ya Elimu kwa Umma na Mafunzo kutoka Tume, Alexander Hassan alisema kuwa hadidu za rejea na muongozo vitasaidia makundi hayo ya haki za binadamu kufanya kazi zake kwa wepesi.

Bw. Victor Rugarabamu, Mwezeshaji kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (WAMJJW), akizungumzia masuala ya mahusiano kati ya Serikali na Asasi za Kiraia (AZAKI)kwenye mkutano uliofanyika tarehe 17-19 Juni, 2019, katika ukumbi wa Cherry Hotel Mjini Morogoro, uliolenga kufanyia tathimini mafanikio, changamoto na matarajio ya makubaliano hayo.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imekutana na Asasi za Kiraia (AZAKI) ilizoingia nazo makubaliano ya kushirikiana kwa lengo la   kujifunza, kubadilishana uzoefu na mawazo ya namna ambavyo taasisi hizo zitakuwa na ushirikiano wenye tija katika utekelezaji wa kazi zao za kila siku.

Akifungua mkutano huo Juni 17, 2019 Mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa Idara ya Elimu kwa Umma na Mafunzo, Alexander Hassan ambaye alimuwakilisha Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora alisema kuwa 

Ni ukweli usiopingika kuwa bila mashirikiano yenye tija miongoni mwa tume  na AZAKI matokeo ya kazi zao hayatawezi kuwa makubwa.

Hivyo mkutano huo umelenga katika kuboresha ushirikiano huo ili uwe na manufaa kwa jamii wanayoihudumia.

THBUB yahamia Dodoma

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inapenda kuujulisha umma wa Watanzania na wadau wake wote kuwa Makao Makuu ya ofisi yamehamia  jijini Dodoma.

Makao Makuu ya ofisi hiyo ambayo awali yalikuwa jijini Dar es salaam yamehamia jijini Dodoma rasmi mwezi Agosti, 2019. 

Kwa sasa Tume ipo Mtaa wa Kilimani na inapatikana  kwa anuani  ifuatayo:

Katibu Mtendaji,

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,

Mtaa wa Kilimani,

S.L.P 1049,

DODOMA.

Barua pepe ni This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. na Tovuti ni www.chragg.go.tz .

 

Aidha, Tume inapenda kuujulisha umma kuwa  kando na ofisi hizo za Makao Makuu zilizopo Mtaa wa Kilimani,ofisi zake nyingine zipo  Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) katika jengo la Wizara ya Katiba na Sheria ghorofa ya kwanza na ya pili.

Hivyo, Tume inatumia fursa hii kuwakaribisha wananchi na wadau wote kufika katika ofisi hizo au kutumia mawasiliano yaliyoandikwa  hapo juu ili kupata huduma.  

 

Na Getrude Alex

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), hivi karibuni ilifanya kikao kazi na mwakilishi wa Asasi ya Kiraia ijulikanayo kwa jina la “CEFA” (Comitato Europeo per la Formazione el’ Agricoltura Onlus)  

Mazungumzo hayo ya siku moja yalilenga kujenga mashirikiano ya kikazi, baina ya THBUB na shirika la CEFA hususani kwenye suala la kukomesha ukatiri  na mauaji kwa  watoto na watu wenye ulemavu wa Ngozi.

More Articles ...

Sign up via our free email subscription service to receive notifications when new information is available.