23
Sat, Jan
1 New Articles

Mkurugenzi Mkaazi wa taasisi ya kimataifa ya National Democratic Institute (NDI) nchini,  Sandy Quimbaya amekutana na uongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na kujadiliana mambo mbalimbali ikiwemo uwezekano wa kushirikiana katika kutoa elimu ya uraia kwa jamii na kufanya ufuatiliaji wa uchaguzi ujao nchini. 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeuahidi ujumbe  kutoka Uganda uliojumuisha wabunge wanne (4) na Maafisa wawili  kutoka Serikali ya Uganda kuwa itashirikiana nao katika mchakato wa maandalizi ya muswada wa kuzuia na kupinga vitendo vya mateso na mauaji ya kutoa kafara binadamu vinavyoendelea nchini humo.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa kushirikiana na Asasi ya Public International Law and Policy Group (PILPG) hivi karibuni imeendesha mafunzo ya uandaaji wa mikakati ya uchechemuzi (advocacy strategies) na mpango kazi wa kuzuia vurugu za kiitikadi (Violence extremism) nchini.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inampa pole Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mh.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Watanzania wote kwa ajali ya Kivuko cha Mv Nyerere iliyotokea tarehe 20 Septemba 2018

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inampa pole Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mh.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Watanzania wote kwa ajali ya Kivuko cha Mv Nyerere iliyotokea tarehe 20 Septemba 2018.

Mnamo Desemba 13, 2017,Kaimu Balozi ( Deputy Chief of Mission) wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Inmi K. Patterson alitembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB ) kwa lengo la kufahamu majukumu na changamoto za Tume, nafasi ya Tume katika kushauri Serikali katika kulinda, kutetea na kukuza hazi za binadamu nchini pamoja na kujua utendaji kazi wa Tume kwa ujumla.

 

          Na Getrude Alex  

Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Bi Mary Massay, ameziasa Asasi za Kiraia (AZAKI) kuzingatia maadili ya kitanzania wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya  kulinda, kukuza na kutetea haki za binadamu nchini.

Akifungua semina ya siku mbili ya kutiliana saini ya ushirikiano baina ya Tume na AZAKI 20, iliyofanyika makao makuu ya THBUB jijini Dar Es Salaam June 6, mwaka huu; Bibi Massay alisema kuwa, AZAKI na watetezi wa haki za binadamu kwa ujumla watakuwa na nafasi kubwa ya kufanikisha malengo yao iwapo watazingatia maadili ya kitanzania hususani matumizi ya lugha ya kistaarabu.

“Ni kitu kibaya  AZAKI kuonekana kama wapinzani au wanaharakati tufanye kazi kwa kuzingatia maadili ya kitanzania, lugha tuzizingatie kweli kweli alisema”

Kwa mujibu wa katibu mtendaji huyo, kama ilivyo kwa baba katika familia akielezwa jambo kwa heshima na anaowaongoza anasikiliza, vivyohivyo AZAKI na watetezi wa haki za binadamu wanayo nafasi kubwa ya kusikilizwa na serikali iwapo watawasilisha madai na mapendekezo yao kwa lugha ya kistaarabu.

“Tume kama chombo huru cha serikali tunaposhirikiana nanyi, tunawatarajia mzingatie sana maadili ya kitanzania” Bibi Massay alisema.

Aidha, Bibi Massay alizitaka AZAKI kutumia mamlaka zao kutoa elimu ya haki za binadamu, kufanya ufuatiliaji na kutoa taarifa za uvunjifu wa haki  hizo hapa nchini.

Hivyo Novemba 2017, THBUB ilizifanyia tathimini Asasi za Kiraia zipatazo 94, zinazojihusisha na masuala ya haki za binadamu nchini. Kati ya hizo AZAKI 20, 18 kutoka bara na 2 visiwani zilikidhi vigezo vya kufanya kazi na Tume na kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano.

Kwa kutambua umuhimu na nafasi za AZAKI katika kukuza, kulinda na kutetea haki za binadamu nchini, Tume imekuwa na mkakati mahususi wa kukuza mashirikiano na AZAKI hizo.

Katika makubaliano hayo yaliyotiwa saini Juni 6, mwaka huu, AZAKI zinategemewa kuwasaidia wananchi ambao haki zao zimevunjwa, kuwasilisha malalamiko yao Tume au kwenye vyombo vinginevyo vilivyowekwa kisheria, kueneza elimu ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa jamii na mtu mmojammoja, kuandaa program za pamoja za uelimishaji umma na kufanya ufuatiliaji wa uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa  misingi ya utawala bora.

 

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora(THBUB), Mheshimiwa Kevin Mandopi amewakumbusha na kuwahimiza wadau wa haki za binadamu umuhimu wa kulinda amani iliyopo nchini.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inaungana na wadau wote wanaolinda na kutetea haki za watu wenye ualbino nchini kwenye kuadhimisha siku ya Kimataifa ya kutoa Elimu kuhusu dhana na haki za watu wenye ualbino duniani “International Albinism Awareness Day’’ tarehe 13/06/2018 ikiwa na kauli mbiu “KUANGAZA MWANGA WETU ULIMWENGUNI”. Kitaifa maadhimisho haya yatafanyika Mkoani Simiyu. 

Siku hii imepitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa Azimio Na. A/HRC/RES/23/13 la terehe 18/12/2014. Tanzania ni mwanachama hai wa Baraza hilo, hivyo kama nchi tunapaswa kuishi tamko la Umoja wa Mataifa kwa vitendo na kutekeleza yaliyokubaliwa

Tume kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini tunaendelea kutetea haki za watu wenye ualbino na kuweka msukumo wa utekelezaji wa Sheria ya Watu wenye Ulemavu ya mwaka 2010.

Watanzania wanatakiwa kuachana na imani potofu za kishirikina za kuwaua, kuwanyanyapaa, kuwabagua na kuwatesa watanzania wenzetu wenye ualbino. Matukio ya ukatili, unyanyasaji, na mauaji kwa watu wenye ualbino yamepungua kwa kiasi nchini. Katika hili Tume inapenda kipekee kutambua juhudi kubwa za Serikali na wadau wote katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa watu wenye ualbino. Wenzetu wenye ualbino wanakabiliwa na changamoto zingine za kielimu, kiafya na kijamii na unyanyapaa ambapo juhudi zaidi kutoka kwa wadau wote zinahitajika. 

Aidha, Tume inaiomba Serikali kuendeleza juhudi zake za kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba (sunscreen lotions) na vifaa saidizi vya kielimu kwa watu wenye ualbino ili waweze kushiriki kikamilifu katika kutoa mchango wao katika kujenga Taifa letu. 

Tume inaahidi kuendelea kushirikiana na wadau wote katika kuhakikisha haki za watu wenye ulemavu wakiwemo watu wenye ualbino zinalindwa, zinakuzwa na kutetewa nchini.  

 

 

Imetolewa na:

 

Mary Massay

KATIBU MTENDAJI

 

 

The Commission for Human Rights and Good Governance is pleased to share the National Baseline Assessment (NBA) Report on Business and Human Rights in Tanzania launched on 9th November, 2017. The NBA provides the current situation of the implementation of the United Nations Guiding Principles (UNGPs) on business and human rights in Tanzania.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), ikiwakilishwa na  Katibu Mtendaji Bi Mary Massay, Mkurugenzi wa Utawala Bora Bi Fatma Muya na  Afisa Uchunguzi Bw. Vicenti Mbombo, imeshiriki mkutano  wa   Omboudsuman   Uliofanyika Djibout, Machi 6 hadi 8, mwaka huu.

Sign up via our free email subscription service to receive notifications when new information is available.