04
Tue, Aug
3 New Articles

Tangazo kwa Umma

Announcements
Typography

Kamati ya Uteuzi ya Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, iliyoundwa na Ibara ya 129(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inautangazia umma kwamba, kwa mujibu wa masharti ya Kifungu cha 7 cha Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Sura ya 391 Toleo la 2002 na Masharti ya Kanuni ya 6 na 7 za Kanuni na Uteuzi wa Makamishna za Mwaka 2001, Waombaji wa Kazi katika nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora waliooredheshwa katika Tangazo hili ndiyo yaliopitishwa na Kamati kwa madhumuni ya kusailiwa.

 Waombaji ambao majina yao hayakuorodheshwa wachukulie kwamba hawakupitishwa.

Kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 7 ya Kanuni za Mwaka 2001, Kamati ya Uteuzi inawaomba wananchi kwa ujumla kuwasilisha maoni yao kuhusu sifa na uwezo wa waombaji waliopitishwa na Kamati. Inasisitizwa kuwa maoni ya wananchi yatashughulikiwa na Kamati kwa njia ya siri.

Siku ya mwisho ya kupokea maoni ya wananchi itakuwa ni tarehe 23 Januari, 2018.

Maoni hayo yawasilishwe kwa njia ya maandishi kwa:

Katibu,

Kamati ya Uteuzi,

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,

Kivukoni Front, (Karibu na Mahakama Kuu ya Tanzania),

S.L.P 9050, DAR ES SALAAM.

 

Au kwa mkono:

Katibu Mtendaji,

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,

Mtaa wa Luthuli, Jengo la Haki Na. 10,

S.L.P 2643, DAR ES SALAAM.

Barua Pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Mwisho wa kuwasilisha maoni ni Januari 23, 2018.

ORODHA YA MAJINA YA WAOMBAJI WALIOPITISHWA

NAFASI YA MWENYEKITI

1. Engera A. Kileo (DODOMA)

2. Gidion Kaino Mandesi (DAR ES SALAAM)

3. Esaka D. N. Mugasa (DAR ES SALAAM)

NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI

1. Muhammad Yussuf (ZANZIBAR)

2. Mohamed Khamis Hamad (ZANZIBAR)

3. Amina Talib Ali (ZANZIBAR)

4. Mwinyiusi A. Hassan (ZANZIBAR)

5. Modest Damian Hassan (ZANZIBAR)

NAFASI YA MAKAMISHNA

1. Muhammad Yussuf (ZANZIBAR)

2. Epiphania H. Mfundo (DAR ES SALAAM)

3. Salum Mohamed Chima (SINGIDA)

4. Rehema Ntimizi (DAR ES SALAAM)

5. Modest Damian Hassan (ZANZIBAR)

6. Mwinyiusi A. Hassan (ZANZIBAR)

7. Albert K. Kakengi (MWANZA)

8. Gidion Kaino Mandesi (DAR ES SALAAM)

9. Dotto Joseph J Nghwelo (DAR ES SALAAM)

10. Amina Talib Ali (ZANZIBAR)

11. Anneth Amin (LUSHOTO)

12. Rashid Khamis Othman (ZANZIBAR)

13. Salma Ali Hassan (ZANZIBAR)

14. Dr. Evaristo Andreas Mtitu (DAR ES SALAAM)

15. Mohamed Khamis Hamad (ZANZIBAR)

16. Nyanda Josiah Shuli (DAR ES SALAAM)

17. James Willy Sillas (MOSHI)

18. Doris Wilson Mangure (TANGA)

19. Said Ali Haji (PEMBA)

20. Maurus Mhakilicha (ZANZIBAR)

21. Dr. Ally Possi (DAR ES SALAAM)

 

Sign up via our free email subscription service to receive notifications when new information is available.