05
Wed, Aug
3 New Articles

THBUB Yalaani Uvamizi wa Studio za Clouds Media

Sufficiently alienation plato scared heights advice

Press Release
Typography

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepata taarifa kupitia vyombo vya habari kuhusu uvamizi wa kituo cha Luninga na Radio cha Clouds Media Group, uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, usiku wa tarehe 17, Machi mwaka huu, akiwa na askari wenye silaha.

 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepata taarifa kupitia vyombo vya habari kuhusu uvamizi wa kituo cha Luninga na Radio cha Clouds Media Group, uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, usiku wa tarehe 17, Machi mwaka huu, akiwa na askari wenye silaha.

 Kwa mujibu wa taarifa hizo, inadaiwa kuwa Mhe. Mkuu wa Mkoa alifika katika studio hizo kwa Iengo Ia kushinikiza kutangazwa kwa taarifa iliyokuwa na maslahi yake binafsi.
Kitendo cha Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam kuvamia kituo cha Clouds Media Group ni kitendo kinachopingana na Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayolinda uhuru wa maoni na mawasiliano, jambo ambalo pia linalindwa na Ibara ya 19 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (1966), na Ibara ya 9 ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu (1986).

Tume imepitia Sheria kadhaa, ikiwemo Sheria ya Tawala za Mikoa Sura ya 97 ya Sheria za Tanzania na imebaini kwamba hakuna Sheria inayomruhusu Mkuu wa Mkoa kuchukua hatua za uvamizi, kama alivyofanya Mhe. Makonda.

Hivyo, hatua ya kuvamia kituo cha habari cha Clouds, akiambatana na askari wenye silaha ni kitendo kisichojali, waIa kuheshimu utawala wa sheria na haki za binadamu. Ni kitendo cha kujichukulia sheria mkononi na kisichokubalika katika jamii au nchi ya kidemokrasia.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inapenda kuungana na Watanzania wengine kulaani kitendo hicho.

Hivyo, Tume inashauri:

1. Mhe. Paul Makonda akiri kuwa kitendo alichofanya ni uvunjifu wa haki za msingi za waandishi wa habari na uhuru wa vyombo vya habari.

2. Kitendo cha kuvamia kituo cha Luninga na Radio cha Clouds Media Group kwa kutumia askari wa Jeshi Ia Polisi kwa maslahi binafsi ni kitendo kisichoendana na utawala wa Sheria, Mhe. Makonda amelidhalilisha Jeshi Ia Polisi, kwa hiyo ni budi awaombe radhi Watanzania.Sign up via our free email subscription service to receive notifications when new information is available.