05
Wed, Aug
3 New Articles

TAMKO LA TUME KUHUSU UBOMOAJI WA NYUMBA ZILIZOJENGWA PEMBEZONI MWA RELI YA KATI, ENEO LA BUGURUNI

Press Release
Typography

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imesikitishwa na kitendo kilichofanywa na Kampuni ya RAHCO cha kubomoa nyumba zaidi ya 200 zilizojengwa pembezoni mwa reli maeneo ya Buguruni siku ya Jumamosi tarehe 11 Machi 2017, baada ya wakazi kutangaziwa ubomoaji huo siku moja kabla, wakati RAHCO wakiwa na taarifa ya wito wa

Tume kuhusu uchunguzi wa malalamiko ya wananchi kuhusu uhalali wa makazi yao kuwa nje ya mita 15 au mita 30 kama Sheria ya Reli, Namba 4 ya mwaka 2002 inavyoelekeza kwa maeneo ya mjini na vijijini.

 

Zoezi hilo Iilianza tarehe 11/03/2017 saa nne asubuhi katika mtaa wa Madenge Kata ya Buguruni, na Iimeendelea tarehe 12/03/2017 katika mitaa ya Faru, Mtakuja na Mtambani katika Kata ya Mnyamani.

Mnamo tarehe 22 Februari 2017 Kamati iIiyoundwa na wanachi wa Mnyamani walifika Tume na kusajili Ialamiko kwamba nyumba zao ziliwekwa alama ya X kuashiria kuvunjwa

bila wao kupewa taarifa, na walipouliza waliambiwa kuwa zitavunjwa tarehe 16 Machi 2017.

Tume iIifanya mawasiliano na Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Mtambani, Faru na Diwani wa Mnyamani kutaka kujua usahihi wa malalamiko ya wananchi, na taarifa za RAHCO

kutaka kuvunja nyumba, Iakini viongozi wa mtaa waliiambia Tume kwamba hawakuwa na taarifa toka RAHCO kama watabomoa nyumba hizo. Tume iIiwasiIiana na RAHCO ambao walisema kwamba eneo hilo ni Ia mradi wa reli ya “Standard gauge” ambao ni mradi muhimu kitaifa na wakadai kuwa ramani ya mipango miji inaonyesha kuwa eneo Ia

Mnyamani Iiko ndani ya mita 30 tofauti na wanachi walivyodai.

Baada ya mawasiliano hayo ya awali Tume iIiiandikia pande zote mbili barua mnamo tarehe 7 Machi 2017 na kuzitaka zilete vielelezo vyao Tume ifikapo tarehe 13 Machi 2017

na ikatoa wito kwa pande zote mbili iIi zifike mbele ya Tume na kusikilizwa tarehe 14 Machi 2017. Baada ya kupata barua ya Tume, RAHCO waliijibu Tume kwamba

wasingeweza kuleta vielelezo eti kwa sababu mwanasheria wao alikuwa safari.

Lakini walikiri kuwa:

 

“Zoezi hilo ambalo lilifanyika kwa mara nyingine tarehe 17 Februari 2017 lilishirikisha wawakilishi mbalimbali kutoka Manispaa, taarifa hiyo iIiwasiIishwa ofisi ya Mkoa na Wilaya

husika. Aidha wawakilishi kutoka Serikali za Mitaa hawakuwepo katika zoezi hilo. Haijulikani ni kwa sababu gani ushiriki wao haukuwepo”. Barua hiyo iIiyopokeIewa Tume

tarehe 9 Machi 2017 ilieleza.

 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inawataka Watanzania na mamlaka kwa ujumla kutambua kwamba, Tume ni taasisi iIiyoundwa ndani ya Katiba ya Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kusimamia haki za binadamu na misingi ya utawala bora. Tume imepewa mamlaka na Katiba kufanya uchunguzi wa malalamiko ya

wananchi kuhusu uvunjifu wa haki za binadamu na misingi ya Utawala Bora.

 

Tume inatambua, kama mwananchi mwingine yeyote, kuhusu umuhimu wa maendeleo ya nchi, umuhimu wa miundombinu ya kisasa ikiwemo reli ya mwendo kasi. Lakini pia

inaamini kuwa iIi utawala wa sheria udumishwe nchini, lazima kiIa mtu na taasisi zote za umma na binafsi ziheshimu utawala wa sheria. Msingi mmoja mkuu wa Utawala Bora ni utii wa sheria.

 

Kwa hiyo, maamuzi na hatua zozote za utekelezaji wa maendeleo ya wananchi yanapochukuliwa lazima yazingatie haki za wananchi. Msingi mkuu wa maendeleo na mlengwa mkuu wa maendeleo ni watu.

 

Tume imesikitishwa na kitenda cha RAHCO kudharau wito wa Tume na kujichukulia sheria mkononi na kuvunja nyumba za wananchi bila kuwapa haki ya kusikilizwa kama

ambavyo Tume iIikwishapanga. Haki hupatikana pande mbili zikisikilizwa, siyo kwa kutumia ubabe wala kwa tafsiri ya sheria ya upande mmoja.

 

Kwa uvunjaji huu uliofanywa na RAHCO, hususani katika eneo Ia Mnyamani, wakati wakijua kuna kikao cha uchunguzi, na kitendo cha kufanya uvunjaji kabla ya siku

wananchi waliyoambiwa, ni uvunjaji wa haki ya msingi ya mtu kupewa muda wa kutosha (notisi), na ni kujichukulia sheria mkononi.

 

Kifungu na 14(2) cha Sheria ya Tume namba 7 ya 2001 Sura 391 kinazitaka mamlaka zinazo Ialamikiwa kushirikiana na Tume kupata ukweli na haki iIipo, na Tume ina wajibu

wa kutoa mapendekezo kwa mujibu wa Katiba, sheria na kanuni husika baada ya kusikiliza pande zote. Tusipofanya haya hatutajenga utamaduni wa kuheshimu, utawala

wa sheria, haki za binadamu na misingi ya utawala bora

 

Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 inatambua haki ya kiIa mtu kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria. Pia Ibara ya 18 (b) inatambua haki ya kila mtu kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu ya jamii. Ibara ya 24 inatambua haki ya kumiliki mali na haki ya hifadhi ya mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria na kunyanganywa mali, ikibidi, kwa mujibu wa sheria. Tanzania ikiwa nchi ambayo imeridhia mikataba ya kimataifa na ya kikanda ya haki za binadamu, inawajibika kulinda haki za wananchi kwa kuhakikisha kwamba hawatendewi vitendo vya kuwadhaiilisha.

 

Uvunjaji wa makazi na uharibifu wa mali za watu uliofanywa na RAHCO, jambo ambalo Iimewatia wananchi wengi ufukara ni kuhatarisha haki ya kuishi ambayo ni haki ya msingi inayotambulika kikatiba, na hata katika sheria za kimataifa. Vitendo hivi (forced eviction) vinapingwa na maazimio na mikataba ya Umoja wa Mataifa ambayo Tanzania

imeyakubali.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inafanya na kusema haya kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, Ibara 130 (1)(c) na (f) vinavyoipa

mamlaka kufanya uchunguzi juu ya mambo yanayohusu uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora; na kuchunguza mwenendo wa mtu yeyote

anayehusika au taasisi yoyote inapokiuka hayo katika utekelezaji wa kawaida wa madaraka ya kazi au majukumu yake.

Tume itaendelea kufanya uchunguzi wake kama ilivyopanga hapo tarehe 14 machi 2017.

Imetolewa na:

 

k.n.y.

Mhe. Bahame Tom Nyanduga

Mwenyekiti

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Machi 13, 2017

Sign up via our free email subscription service to receive notifications when new information is available.