Kukamatwa kwa Mfanyakazi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti na Wenzake

Kukamatwa kwa Mfanyakazi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),Tito Magoti na Wenzake

Press Release
Typography

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepata taarifa kupitia vyombo vya habari, za kutekwa kwa Afisa wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bw. Tito Magoti kuanzia ijumaa Disemba 20, 2019.

Hata hivyo, baadae taarifa zilizopatikana kupitia vyombo vya habari zilimnukuu kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam wa Jeshi la Polisi, SACP, Lazaro Mambosasa akiueleza umma kuwa Afisa huyo anashikiliwa pamoja na wengine watatu(3) kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi kwa tuhuma ya makosa ya jinai ambayo hayakuwekwa wazi. Soma zaidi