Ujumbe wa THBUB Siku ya Maji, Machi 22, 2020

Ujumbe wa THBUB Siku ya Maji, Machi 22, 2020

Press Release
Typography

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana  na Watanzania wote katika kuadhimisha Siku ya Maji Duniani ambayo leo Machi 22, 2020 ndio kilele chake.

Tume inatambua kuwa  haki ya maji ni miongoni mwa haki za kijamii  kama ilivyo haki nyingine, hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa watanzania wanaendelea kufurahia haki hiyo kwa uhakika.

Tume inatambua na inapongeza  jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha watanzania wanaendelea kupata  maji safi na salama.

Kama kauli Mbiu ya mwaka huu inavyosema Maji na Mabadiliko ya Tabia nchi: Uhakika wa Maji Salama kwa wote. Tume inapenda kutoa rai kwa watanzania wote kuendelea kuheshimu na kutunza vyanzo vyote vya maji ikiwemo na  miundo mbinu iliyopo  ili kuisaidia Serikali kuweza kufikisha huduma hiyo kwa kila mwananchi.

Aidha, Tume inatambua kuwa kutokana na Mlipuko wa maradhi ya Ugonjwa wa Korona duniani, Serikali imechukua tahadhari kadhaa ikiwemo kusitisha shughuli mbalimbali zinazoambatana na maadhimisho haya, tume inaunga mkono uamuzi huo ambao unalenga katika  kulinda haki ya afya kwa wananchi.

Kwa msingi huo, Tume inashauri mamlaka husika na Watanzania kwa ujumla kutumia wakati huu kwa kila mmoja kutafakari kwa kina namna bora ya kulinda vyanzo vyote vya maji pamoja na miundo mbinu iliyopo ili sisi wote tuweze kufaidika na rasilimali hii muhimu ambayo ni msingi wa uhai wa mwanadamu.

 

Jaji Mst. Mathew Mwaimu, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Machi 22, 2020.