Pongezi kwa Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria

Press Release
Typography

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inampongeza Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mbunge wa Iramba Magharibi) kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Tume ikiwa taasisi iliyo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria inamkaribisha na inamtakia kila la heri katika majukumu yake hayo mapya.

Aidha, Tume inachukua nafasi hii kumhakikishia kila aina ya ushirikiano atakaouhitaji ili aweze kutimiza majukumu yake wakati wote wa uongozi wake kama Waziri wa Katiba na Sheria.

    Imetolewa na:

 

  (SIGNED)

 Jaji (Mst) Mathew Pauwa Mhina Mwaimu

 Mwenyekiti

  TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Mei 03, 2020