28
Thu, Jan
1 New Articles

Kupongeza juhudi za Serikali dhidi ya Mapambano ya Mlipuko wa Maradhi yanayosababishwa na virusi vya Corona

Itakumbukwa kuwa katikati ya mwezi Machi mwaka huu Serikali ilitangaza mapambano rasmi dhidi ya maradhi yanayosababishwa na virusi vya Corona ambavyo hivi karibuni imekuwa ni janga kubwa duniani.Soma zaidi

 

Ujumbe wa THBUB Siku ya Maji, Machi 22, 2020

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana  na Watanzania wote katika kuadhimisha Siku ya Maji Duniani ambayo leo Machi 22, 2020 ndio kilele chake.

Tume inatambua kuwa  haki ya maji ni miongoni mwa haki za kijamii  kama ilivyo haki nyingine, hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa watanzania wanaendelea kufurahia haki hiyo kwa uhakika.

Kukamatwa kwa Mfanyakazi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),Tito Magoti na Wenzake

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepata taarifa kupitia vyombo vya habari, za kutekwa kwa Afisa wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bw. Tito Magoti kuanzia ijumaa Disemba 20, 2019.

Hata hivyo, baadae taarifa zilizopatikana kupitia vyombo vya habari zilimnukuu kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam wa Jeshi la Polisi, SACP, Lazaro Mambosasa akiueleza umma kuwa Afisa huyo anashikiliwa pamoja na wengine watatu(3) kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi kwa tuhuma ya makosa ya jinai ambayo hayakuwekwa wazi. Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 Tunapoadhimisha kumbukumbu ya siku ya Mwanamke Duniani  hii leo Machi 8, 2020 ikiwa ni miaka 25 tangu wanawake kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wakutane jijini Beijing, China kujadili maendeleo ya wanawake,Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inapenda kuungana na Watanzania wote katika kusherehekea maadhimisho haya ambayo kimsingi yanatoa fursa kwa wanawake kufanya marejeo ya hatua mbalimbali zilizofikiwa katika kuboresha mustakabali wa wanawake nchini.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Itakumbukwa kuwa Desemba, 9, 2019 katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru, Mheshimiwa  Rais John Magufuli alitangaza msamaha na kuwaachia huru wafungwa 5,533.

Uamuzi huo wa Rais wa kuwasamehe wafungwa alioutoa wakati akihutubia wananchi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza umekuwa ukitekelezwa na wakuu wa nchi tangu tupate uhuru mwaka 1961. Hata hivyo, uamuzi wa Rais kuwasamehe wafungwa 5533 ni wa kipekee tangu Tanzania ipate uhuru kutokana na idadi kubwa ya wafungwa aliowasamehe.Soma zaidi

 

THBUB yafanyia kazi ombi la Spika Ndugai

Ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) umefanya ziara ya siku mbili kutembelea Gereza la Kongwa na Gereza la Mpwapwa kufuatilia changamoto zinazokabili Magereza ya Wilaya hizo mbili zilizopo jijini Dodoma.

Ziara hiyo ya THBUB imefanyika kufuatia mazungumzo ya Novemba 19, 2019 kati ya Ujumbe wa THBUB ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu  na  Spika Job Ndugai yaliyofanyika katika ofisi yake ya jimbo iliyopo Wilayani Kongwa jijini Dodoma. Soma zaidi

 

Pongezi kwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli kwa kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani

Itakumbukwa kuwa mapema wiki hii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi watatu wa vyama vya upinzani. 

Kama tunavyofahamu kuwa siku ya Jumapili Novemba 24, 2019 Watanzania kote nchini watafanya uchaguzi wa viongozi ngazi ya Serikali za Mitaa. Hatua hiyo ya uchaguzi imetanguliwa na uandikishaji wapiga kura, uteuzi wa wagombea na kampeni za wagombea, hatua ambazo zimetekelezwa kwa mafanikio makubwa.

 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeridhishwa na idadi ya watu waliojitokeza kujiandikisha kupiga kura. Idadi hiyo imeongezeka ukilinganisha na idadi ya watu waliojiandikisha katika uchaguzi kama huo uliofanyika mwaka 2014.Soma Zaidi

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)inasikitishwa na kauli zinazotolewa na baadhi ya viongozi na makundi ya kisiasa zinazoashiria uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora nchini.Aidha ,kauli hizo zimekuwa zikichochea kwa kiasi kikubwa wanannchi kujichukulia sheria mikononi mwao kutokana na kutoridhishwa na vitendo vya baadhi ya wanasiasa.Soma zaidi

 

More Articles ...

Page 2 of 3
Sign up via our free email subscription service to receive notifications when new information is available.