19
Tue, Jan
1 New Articles

Crime affected citizen thoughts

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepata taarifa kupitia vyombo vya habari kuhusu uvamizi wa kituo cha Luninga na Radio cha Clouds Media Group, uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, usiku wa tarehe 17, Machi mwaka huu, akiwa na askari wenye silaha.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imesikitishwa na kitendo kilichofanywa na Kampuni ya RAHCO cha kubomoa nyumba zaidi ya 200 zilizojengwa pembezoni mwa reli maeneo ya Buguruni siku ya Jumamosi tarehe 11 Machi 2017, baada ya wakazi kutangaziwa ubomoaji huo siku moja kabla, wakati RAHCO wakiwa na taarifa ya wito wa

Tume kuhusu uchunguzi wa malalamiko ya wananchi kuhusu uhalali wa makazi yao kuwa nje ya mita 15 au mita 30 kama Sheria ya Reli, Namba 4 ya mwaka 2002 inavyoelekeza kwa maeneo ya mjini na vijijini.

Despair copy implications shouldn't weren't

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana na wadau wote wa haki za watoto duniani katika kuadhimisha “Siku ya mtoto wa Afrika”. Siku hii inaikumbusha dunia juu ya mauaji ya watoto wapatao 2,000 wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini, waliouawa kikatili miaka 41 iliyopita na iliyokuwa Serikali ya Makaburu.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ,iliandaa mkutano leo tarehe 10/08/2016 ili kuzungumzia tamko la jeshi la Polisi la tarehe 07/06/2016 la kuzuia mikutano na maandamano ya vyama vya siasa isiyo ya kiutendaji ,na tamko la CHADEMA kuhusu "UKUTA"na mikutano wanayopanga kufanya tarehe 01 Septemba,2016.Pakua Habari kamili.

Canada reader forget shaking favorite

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa na taarifa ya kuuwawa kwa aliyekuwaOfisa Upelelezi Mkuu wa Polisi (OC CID) wa Wilaya ya Kibiti na wananchi wengine wawili ambao ni aliyekuwa Mkanguzi wa Maliasili na Mlinzi wa katika Kizuizi cha Maliasili kilichopo katika Kijiji cha Jaribu, Wilaya ya Kibiti, Mkoani Pwani, tukio Iinalodaiwa kufanywa na kundi Ia watu wanaohisiwa kuwa ni majambazi waliovamia Kizuizi hicho usiku wa tarehe 21 Februari, 2017.

Tume inalaani vikali mauaji haya ya kikatili ya watu wasio na hatia. Aidha, tunaungana na Watanzania wengine nchini kuwapa pole wafiwa na wote walioguswa na msiba huu.
Kwa mujibu wa ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, kila mtu anayo Haki ya Kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake kutoka katika jamii, kwa mujibu wa sheria. Hivyo, kuuwawa kwa askari polisi na maafisa hawa ambao walikuwa wakitekeleza majukumu yao kisheria ni kitendo kinachopaswa kuIaaniwa vikali na kiIa
mwananchi.
Kumbukumbu zinaonesha kuwa uvamizi wa vituo na kuuwawa kwa polisi ni matukio yanayojirudia hususan katika Mkoa wa Pwapi, raia wasio wema wamekuwa wakitenda vitendo hivi vya ukatili dhidi ya polisi na raia na kusababisha hofu kubwa miongoni mwa askari, familia zao pamoja na wananchi kwa ujumla.
Hivyo, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inaungana na Serikali katika kukemea vitendo hivi na kuitaka kufanyika uchunguzi wa kina iIi kubaini vyanzo na kupata majawabu sahihi ya matukio na vitendo hivi dhalimu ili kuvidhibiti mapema na hivyo kuwahakikishia askari na raia usalama wao.
Pia, Tume inapenda kuwakumbusha wananchi, na taasisi zote umuhimu wa kupiga vita matendo yote yanayokiuka Sheria, ukiukwaji wa misingi ya utawala wa sheria na haki za binadamu, kwani haya yasipozingatiwa amani na utulivu nchini utatoweka.
Mwisho, Tume inatoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi Ia Polisi katika kuhakikisha watui waliofanya tukio hili wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo husika iIi sheria ichukue mkondo wake.
Imetolewa na:

Mhe. Bahame Tom Nyanduga
Mwenyekiti
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Februari 23, 2017

 

 

 

Page 3 of 3
Sign up via our free email subscription service to receive notifications when new information is available.