Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa na vitendo vya baadhi ya wananchi kuwatumia Watu Wenye Ulemavu kwa kuwafanya ombaomba mitaani kwa lengo la kujiingizia kipato. Aidha, wamekuwa wakiwafanyia vitendo vingine vingi vya udhalilishaji.Soma zaidi
THBUB yakutana na wadau kujadili taarifa ya ukaguzi wa Magereza na Vituo vya Polisi nchini

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Jaji mstaafu Mathew Mwaimu (katikati) pamoja na Makamu wake, Mhe. Mohamed Khamis Hamad (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao cha kujadili taarifa ya Tume ya ukaguzi wa magereza na vituo vya polisi. Wengine kutoka kushoto (waliokaa) ni: Mwakilishi wa Inspekta Jenerali wa Polisi, DCP Fredenand Mtui, Mwakilishi wa Ofisi ya Msajili Mkuu Mahakama ya Rufani, Mhe. Silvia Lushasi na Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Burton Mwasomola. Kikao hicho cha siku moja kimefanyika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma leo Desemba 8, 2020.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Jaji mstaafu Mathew Mwaimu (katikati) pamoja na Makamu wake, Mhe. Mohamed Khamis Hamad (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao cha kujadili taarifa ya Tume ya ukaguzi wa magereza na vituo vya polisi. Wengine kutoka
UNDP yaipongeza Tume kwa ukuzaji wa haki za binadamu nchini

Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bibi Christine Musisi akimkabidhi Mwenyekiti wa THBUB, Jaji (mstaafu) Mathew Mwaimu mojawapo ya vifaa vilivyotolewa kama msaada.
SHIRIKA la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) limetoa pongezi kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa hatua inazochukua kulinda na kukuza haki za binadamu na misingi ya utawala bora hapa nchi.
Tamko la THBUB Siku ya watu wenye ulemavu duniani

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Mathew Mwaimu (Jaji Mstaafu) akitoa tamko la Tume mbele ya vyombo vya habari kuadhimisha Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani ofisini kwake jijini Dodoma leo Desemba 3, 2020
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana na wadau wote wa haki za Watu Wenye Ulemavu duniani katika kuadhimisha “Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu” ikiwa na kauli mbiu “Si Kila Ulemavu Unaonekana”.Soma zaidi Soma zaidi
Taasisi za utawala bora zashauriwa kushirikiana

Mwenyekiti wa THBUB, Jaji (Mst) Mathew Mwaimu (kulia) akiongea na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma, Jaji (Mst) Harold Nsekela (Kushoto) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma jana. Lengo la ziara hiyo ya THBUB ni kuimarisha ushirikiano na Sekretarieti ya Maadili
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma, Jaji (Mst) Harold Nsekela amezishauri taasisi zinazosimamia utawala bora kushirikiana kwa karibu ili waweze kutekeleza majukumu yao vizuri.
Jaji Nsekela alitoa rai hiyo katika ofisi yake jijini Dodoma jana alipokutana na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji (Mst) Mathew Mwaimu.
MAADHIMISHO YA KILELE CHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI.

Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tulia Ackson (kushoto) akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Mohamed Khamis cheti cha kutambua mchango wa Tume katika kuwawezesha Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kutimiza majukumu yao. Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wauguzi Duniani yalifanyika hospitalini hapo jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. (Mei 15, 2020).
Tamko la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kuhusu Uchaguzi Mkuu 2020
OKTOBA 28, 2020 Watanzania wote waliotimiza vigezo kwa mujibu wa sheria, wanatarajia kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura kuwachagua Rais, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani. Hatua hii muhimu imefikiwa baada ya kukamilika kwa mchakato wa miezi kadhaa uliohusisha hatua za uhuishaji wa madaftari ya kudumu ya wapiga kura, uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali na kampeni.Soma zaidi
Kusikitishwa na Taarifa ya vitendo vya baadhi ya Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ,Mwananyamala Kuwanyanyapaa na kuwasumbua Wagonjwa
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa na Taarifa ya vitendo vinavyofanywa na baadhi ya Madaktari ana Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Mwananyamala vya kuwanyanyapaa na kuwasubua wagonjwa hao kwenda kufanya vipimo vya Korona kabla ya kuanza kupata matibabu.Soma zaidi
TAMKO LA THBUB WAKATI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI OKTOBA MOSI, 2020
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana na wadau wote duniani kuadhimisha siku ya wazee duniani yanayofanyika kila ifikapo tarehe Mosi Oktoba ya kila mwaka. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu inasema “Familia na Jamii Tuwajibike kuwatunza Wazee.”Soma zaidi
Salamu za Pole kwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepokea kwa mshituko mkubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga (Mb) kilichotokea leo alfajiri Mei 01, 2020 Jijini Dodoma.
Tume inatoa pole kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuondokewa na kiongozi mchapakazi, mwadilifu, mzalendo na mwanadiplomasia mahiri aliyeiwakilisha na kuipigania Tanzania katika nyanja za Kimataifa kwa miaka mingi.Soma zaidi