19
Tue, Jan
1 New Articles

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Tahadhari dhidi ya Kusambaa kwa Virusi vya Corona

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa kuzingatia tamko la Serikali kuhusu tahadhari ya kusambaa kwa ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya Corona, inatoa mwongozo ufuatao, unaopaswa kuzingatiwa na wananchi wote wanaofika katika ofisi za Tume kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali:-Soma Zaidi

 

Mkurugenzi wa HUPEMEF, Mchungaji Saimon Chemu (Kulia) akitoa maelezo mafupi kwa Mwenyekiti wa THBUB, Jaji (Mst.) Mathew Mwaimu (Kushoto) alipotembelea ofisi za Taasisi hiyo zilizopo Wilayani Magu, jijini Mwanza Aprili 21, 2020.

Na Mbaraka Kambona

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji (Mst.) Mathew Mwaimu amezitaka taasisi zilizoingia  mkataba wa ushirikiano na Tume kuendeleza jitihada za kusaidia wananchi ili kutatua kero zinazowakabili katika maeneo yao.

Jaji Mwaimu alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano baina ya THBUB na Taasisi ya Huruma, Peace and Mercy Foundation (HUPEMEF) uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo zilizopo Wilayani Magu, Mkoani Mwanza Aprili 21, 2020.

Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa (kulia) akiongea na Mwenyekiti wa THBUB, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma leo Februari 24, 2020. Ambapo pamoja na mambo mengine alipongeza uamuzi wa Rais John Magufuli wa kuwateua Makamishna hao wa tume.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) nchini umepongeza hatua ya Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ya kuwateua Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB).

Pongezi hizo zimetolewa na Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao  huo, Onesmo Olengurumwa alipokutana na Mwenyekiti wa THBUB, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu ofisini kwake jijini Dodoma leo Februari 24, 2020.

Mwenyekiti wa THBUB, Jaji (Mst.) Mathew Mwaimu (katikati) akiongea wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia) ofisi kwake jijini Mwanza Aprili 20, 2020. Kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa THBUB, Hajjat Fatma Muya.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella ameishauri Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kuandaa mpango maalamu wa kutoa elimu ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora  kwa Watendaji wa ngazi za mikoa ili waweze kutoa haki za  wananchi kwa wakati. 

Mongella alitoa rai hiyo katika kikao kifupi kilichofanyika baina yake na Mwenyekiti wa THBUB, Jaji (Mst.) Mathew Mwaimu alipomtembelea  ofisini kwake  jijini Mwanza Aprili 20, 2020.

Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Kimarekani, USAID, Andy Karas akiongea katika kikao kifupi kilichofanyika baina yake na viongozi wa tume alipotembelea ofisi hizo za THBUB zilizopo jijini Dodoma leo (Februari 20, 2020).

Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Kimarekani nchini Tanzania, USAID, Andy Karas ameipongeza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa jitihada zake za kujenga jamii inayoheshimu na kuzingatia haki za binadamu na misingi ya utawala bora, na kusema kuwa jitihada hizo ni muhimu katika kusaidia nchi kufikia malengo yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikiapo 2025.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji (Mst.) Mathew Mwaimu akiwasilisha taarifa ya THBUB kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika warsha iliyoandaliwa Mkoani Morogoro na THBUB kwa kushirikiana na Haki Maendeleo . Katikati ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka, wa kwanza kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dk Augustine Mahiga.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imeiagiza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa kushirikiana na Taasisi ya Haki Maendeleo kuandaa mapendekezo yatakayosaidia kuanzishwa kwa mchakato wa  kutungwa kwa sheria ya kulinda haki za mtumiaji wa huduma za mifumo ya kimtandao na kuyawasilisha kwa kamati hiyo ili waweze kushawishi bunge na mamlaka nyingine husika ili sheria hiyo iweze kutungwa.

Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mette N. Dissing-Spandet akiongea na Mwenyekiti wa THBUB, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu katika mazungumzo yaliyofanyika kwenye ofisi za THBUB jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.

Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mette N. Dissing-Spandet, ameieleza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kuwa wataendelea kufanyakazi kwa karibu na tume kufuatia  mahusiano mazuri ya muda mrefu yaliyojengeka baina  ya Denmark na Tanzania.

Dissing-Spandet alitoa ahadi hiyo katika mazungumzo yaliyofanyika kwenye ofisi za THBUB jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma baina yake na Mwenyekiti wa THBUB, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu.

Alisema kuwa Denmark itaendelea kufanya kazi na THBUB na itaendelea kuisaidia kutekeleza majukumu yake ya kuhamasisha, kutetea na kulinda haki za binadamu nchini.

“Denmark imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na THBUB kwa muda mrefu sasa, na tupo tayari kuendeleza ushirikiano wetu, tumeweza kufanya kazi kwa karibu kutokana na mahusiano mazuri ya muda mrefu baina ya nchi zetu mbili”, alisema  Dissing-Spandet

Kwa mujibu wa Balozi huyo,  alisema kuwa ni muhimu katika nchi yoyote kuwa na taasisi kama THBUB kwa kuwa zinasaidia nchi katika kuhamasisha uzingatiwaji wa masuala ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

Mwenyekiti wa THBUB, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu alionesha kuridhishwa kwake na ushirikiano ulipo baina ya tume na Denmark na kusema kuwa  ushirikiano huo umesaidia sana tume kuweza kutimiza majukumu yake kwa kiasi kikubwa.

“Tunashukuru kwa jitihada zenu za dhati za kutuunga mkono, Denmark mmekuwa washirika wa mwanzo kabisa kuisaidia tume, na kupitia msaada wenu tume iliweza kujenga jengo hili la Haki House ambalo ndio tumekuwa tukilitumia kama ofisi zetu...Ahsante sana”, Jaji Mwaimu alimshukuru Balozi huyo

Kamishna wa THBUB, Nyanda Shuli alisema katika kikao hicho kuwa moja ya mipango ya THBUB mwaka huu ni kufanya ufuatiliaji wa uchaguzi mkuu utakaofanyika baadae mwaka huu, na kwamba mpaka sasa wameshaanza kufuatilia mchakato wa daftari la mpiga kura.

“Miongoni mwa mipango yetu mwaka huu wa uchaguzi ni kuwa na mikutano ya majadiliano na wadau mahususi ikiwemo Jeshi la Polisi, Vyama vya Siasa na Tume ya Uchaguzi ili kukumbushana umuhimu wa kuwa na uchaguzi wa amani nchini”, alieleza Shuli

Ziara ya Balozi huyo kwa tume ni ya kwanza ambayo ililenga katika kufahamiana na kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya THBUB na Denmark katika kuimarisha uzingatiwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora nchini. .  

 

 ---Mwisho---

 

Ujumbe wa THBUB ukiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Enid Chiwanga (katikati) huku wakionyesha ishara ya “mwanamke hodari”muda mfupi mara baada ya ujumbe wa THBUB kumaliza ziara yake katika hospitali hiyo.

Katika kuelekea kilele cha kuadhimisha siku ya wanawake duniani, ujumbe wa wanawake kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) umetembelea Idara ya Magonjwa ya Wanawake na Uzazi iliyopo katika  Hospitali ya rufaa  jijini Dodoma mapema leo Machi 6, 2020.

Ujumbe huo  uliotembelea  hospitali hiyo uliongozwa na Makamishna wawili, Dkt. Fatma Khalfan na Amina Talib Ali kwa lengo la kuwafariji wakina mama wagonjwa na wazazi waliolazwa katika hospitali hiyo. 

Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Paul Sherlock (wa pili kushoto) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa THBUB, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (katikati) muda mfupi baada ya kikao chao katika ofisi za ubalozi huo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Aran Corrigan, Mtaalamu Mwandamizi wa Jinsia na Utawala Bora wa ubalozi wa Ireland, na wa pili kulia ni Kamishna wa THBUB, Nyanda Shuli. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango wa THBUB, Laurent Burilo

Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Paul Sherlock  ameonesha nia ya kushirikiana na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) katika kutoa elimu ya kukuza uelewa wa wananchi kuhusu  haki za binadamu na misingi ya utawala bora nchini. 

Sherlock alionesha utayari huo wa kushirikiana na THBUB wakati wa mazungumzo yake na ujumbe wa tume, ulioongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu ulipomtembelea katika ofisi zake jijini Dar es Salaam Februari 13, 2020.

Wakati akijibu  ombi la Mwenyekiti wa tume ambapo alimuomba kuangalia uwezekano wa kushirikiana katika kuelimisha wananchi wa Tanzania kuhusu haki ya ardhi, Balozi alisema kuwa hilo ni jambo zuri na wataangalia uwezekano huo.

Kwa mujibu wa Jaji Mwaimu, maeneo mengi nchini kuna migogoro ya ardhi, huku akitaja baadhi ya maeneo kama ya Kilosa na Kilombero kama mfano wa maeneo yenye migogoro, na kusema kuwa wanawake ndio wahanga wakubwa linapokuja suala la umiliki wa ardhi.

“Nafikiri hilo litakuwa jambo zuri,  tutakaa tuone namna bora tunaweza kushirikiana katika kazi hiyo ambayo ipo katika mamlaka yenu, tutajadiliana na kuona wapi tunaweza kushirikiana”, alisema Sherlock

Akiongea mapema katika kikao hicho, Kamishna wa Tume, Nyanda Shuli alisema kuwa kwa sasa THBUB inapokea malalamiko mengi yanayohusu mafao, watu kuachishwa kazi bila kuzingatia taratibu, Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Paul Sherlock  ameonesha nia ya kushirikiana na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) katika kutoa elimu ya kukuza uelewa wa wananchi kuhusu  haki za binadamu na misingi ya utawala bora nchini. 

Sherlock alionesha utayari huo wa kushirikiana na THBUB wakati wa mazungumzo yake na ujumbe wa tume, ulioongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu ulipomtembelea katika ofisi zake jijini Dar es Salaam Februari 13, 2020.

Wakati akijibu  ombi la Mwenyekiti wa tume ambapo alimuomba kuangalia uwezekano wa kushirikiana katika kuelimisha wananchi wa Tanzania kuhusu haki ya ardhi, Balozi alisema kuwa hilo ni jambo zuri na wataangalia uwezekano huo.

Kwa mujibu wa Jaji Mwaimu, maeneo mengi nchini kuna migogoro ya ardhi, huku akitaja baadhi ya maeneo kama ya Kilosa na Kilombero kama mfano wa maeneo yenye migogoro, na kusema kuwa wanawake ndio wahanga wakubwa linapokuja suala la umiliki wa ardhi.

“Nafikiri hilo litakuwa jambo zuri,  tutakaa tuone namna bora tunaweza kushirikiana katika kazi hiyo ambayo ipo katika mamlaka yenu, tutajadiliana na kuona wapi tunaweza kushirikiana”, alisema Sherlock

Akiongea mapema katika kikao hicho, Kamishna wa Tume, Nyanda Shuli alisema kuwa kwa sasa THBUB inapokea malalamiko mengi yanayohusu mafao, watu kuachishwa kazi bila kuzingatia taratibu, upatikanaji wa haki kwa wakati na malalamiko kuhusu migogoro ya ardhi.  

Nyanda alisema kufuatia hali hiyo, THBUB inajipanga kujikita katika kuandaa mbinu zitakazo saidia kutoa majawabu ya matatizo hayo.

“ katika utatuzi wa migogoro tume tunahimiza kukaa katika mazungumzo ili kupata ufumbuzi, sisi tunaamini katika kuleta watu pamoja na kuzungumza kuhusu matatizo yao na kuyapatia ufumbuzi”, alisema Shuli

Kaimu katibu Mtendaji wa THBUB, Hajjat Fatuma Muya alieleza katika kikao hicho kuwa tume imekuwa ikifanya kwa karibu na taasisi mbalimbali za ndani na za kimataifa likiwemo Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Aidha, Muya alisema kuwa tume imeingia mkataba wa ushirikiano na AZAKI ishirini na moja (21) nchini kwa lengo la kuunganisha nguvu ili kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa, zinakuzwa na kuheshimiwa.

Aliendelea kueleza kuwa kupitia ushirikiano huo, hivi Karibuni THBUB kwa kushirikiana na taasisi ya Haki Maendelea walitoa mafunzo ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa Madiwani ishirini na saba (27) wa Halmashauri ya Mkoa wa Lindi.

Ziara ya THBUB katika ubalozi wa Ireland ililenga katika kujenga mahusiano na na kutafuta ushirikiano wa kikazi kwa muelekeo wa kuhakikisha kuwa haki za binadamu na misingi ya utawala bora inatunzwa na kuheshimiwa nchini.

---MWISHO---

upatikanaji wa haki kwa wakati na malalamiko kuhusu migogoro ya ardhi.  

Nyanda alisema kufuatia hali hiyo, THBUB inajipanga kujikita katika kuandaa mbinu zitakazo saidia kutoa majawabu ya matatizo hayo.

“ katika utatuzi wa migogoro tume tunahimiza kukaa katika mazungumzo ili kupata ufumbuzi, sisi tunaamini katika kuleta watu pamoja na kuzungumza kuhusu matatizo yao na kuyapatia ufumbuzi”, alisema Shuli

Kaimu katibu Mtendaji wa THBUB, Hajjat Fatuma Muya alieleza katika kikao hicho kuwa tume imekuwa ikifanya kwa karibu na taasisi mbalimbali za ndani na za kimataifa likiwemo Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Aidha, Muya alisema kuwa tume imeingia mkataba wa ushirikiano na AZAKI ishirini na moja (21) nchini kwa lengo la kuunganisha nguvu ili kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa, zinakuzwa na kuheshimiwa.

Aliendelea kueleza kuwa kupitia ushirikiano huo, hivi Karibuni THBUB kwa kushirikiana na taasisi ya Haki Maendelea walitoa mafunzo ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa Madiwani ishirini na saba (27) wa Halmashauri ya Mkoa wa Lindi.

Ziara ya THBUB katika ubalozi wa Ireland ililenga katika kujenga mahusiano na na kutafuta ushirikiano wa kikazi kwa muelekeo wa kuhakikisha kuwa haki za binadamu na misingi ya utawala bora inatunzwa na kuheshimiwa nchini.

---MWISHO---

 

Mwenyekiti wa THBUB, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu akiongea katika kikao cha majadiliano kilichowakutanisha ujumbe wa THBUB na Viongozi wa LHRC kwenye ofisi za kituo hicho jijini Dodoma leo (Februari 27, 2020). Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)  wamekubaliana kuandaa mpango wa pamoja wa kutoa elimu katika mashuleni   ili kuhamasisha na  kukuza  haki za binadamu nchini.

Makubaliano hayo yalifikiwa na pande zote mbili baada ya majadiliano yaliyofanyika katika kikao kilichowakutanisha ujumbe wa THBUB na Viongozi wa LHRC kwenye ofisi za kituo hicho jijini Dodoma leo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Rehema Madenge akiongea wakati akiukaribisha ujumbe wa THBUB na Viongozi wa Haki Maendeleo walipotembelea ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Lindi. Kulia Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeshauriwa kujikita katika kutoa elimu ya haki ya ardhi na mirathi kwa kuwa maeneo hayo yameonekana kuwa na changamoto kubwa sana kwa jamii nchini.

Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alipokutana na ujumbe wa THBUB na viongozi wa Asasi ya kiraia, Haki Maendeleo walipomtembelea ofisini kwake kumpa pole kufuatia maafa waliyoyapata yaliyosababishwa na  mafuriko ya mvua yaliyotokea mkoani humo hivi karibuni.

Akiongea katika kikao hicho kilichofanyika leo Februari 8, 2020 katika ofisi zake mkoani Lindi, RC Zambi  alisema kuwa tume iwaelimishe wananchi kuhusu haki zao ili wazijue na waeleweshwe taratibu za kufuata pindi wanapotaka kudai haki zao zitakapokuwa zimevunjwa.

Alisema kuwa shida  ipo kwa wananchi wa chini ambao kwa kiasi kikubwa hawajui haki zao na hata ikitokea kuwa wanazifahamu bado hawajui njia sahihi za kufuata pale haki yake inapokuwa imevunjwa ili kuidai.

Aliendelea kusema kuwa matatizo mengi yapo katika ardhi na mirathi hivyo aliishauri tume kutoa elimu zaidi katika maeneo hayo ili watu wajue haki zao na njia za kufuata pindi wanapotaka kudai haki zao.

“Kwenye mirathi huko kuna matatizo, watu hawajui haki zao, ardhi pia kuna shida sana lakini wananchi hawajui njia za kufuata kudai haki zao, tuwasaidie wananchi hawa ili wajue njia za kufuata kudai haki zao ”, alisema Zambi

“Mheshimiwa Rais Magufuli anatuambia kila siku kuwa ametutuma ili tukatatue kero za wananchi, tena wananchi wa chini”,aliongeza 

“Tunatambua kuwa tume hamuwezi kwenda kila mahali, sisi tupo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi kutatua kero zao, hivyo tushirikiane katika kutatua kero hizo”, alisisitiza 

Kamishna wa THBUB, Amina Talib Ali, ambaye ndiye alikuwa mkuu wa msafara huo alimueleza mkuu wa mkoa kuwa tume imekuwa ikifanya kazi zake kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo za serikali, binafsi na taasisi za kimataifa katika kuhakikisha haki za binadamu na misingi ya utawala bora inalindwa na kukuzwa nchini.

Amina alimueleza mkuu wa mkoa kuwa itaendele kushirikiana na wadau wote katika kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa na kuzingatiwa. Hata hivyo, Katika kuimalisha ushirikiano huo Kamisha alimueleza mkuu wa Mkoa kuwa  wametoa mafunzo kwa Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya mkoa huo wa Lindi ili kuwajengea uwezo wa masuala ya haki za binadamu na utawala bora. Mafunzo hayo yalitolewa na THBUB kwa kushirikiana na Asasi ya Kiraia, Haki Maendeleo ambayo ndio iliwezesha mkutano huo kufanyika.

Kikao hicho cha Mkuu wa Mkoa  na THBUB pamoja na viongozi wa Haki Maendeleo pia kilihudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkao wa Lindi, Rehema Madenge na Wakuu wa Wilaya tano za Mkoani humo.

---Mwisho---

 

More Articles ...

Sign up via our free email subscription service to receive notifications when new information is available.