28
Thu, Jan
1 New Articles

Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu, Zanzibar, Omary Othman Makungu (katika) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa THBUB, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu(kulia kwake) na Viongozi wengine wa tume. Mwenyekiti wa tume alimtembelea Jaji Mkuu ofisini kwake Desemba 2, 2019.

Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu, Visiwani Zanzibar, Omary Othman Makungu amemueleza Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu kuwa wako tayari kushirikiana tume kutatua kero za wananchi zinazohusu upatikanaji wa haki nchini.

Jaji  Makungu alisema hayo alipokutana na Mwenyekiti wa tume ofisini kwake Visiwani Zanzibar Desemba 2, 2019. 

Mwenyekiti wa THBUB Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu akiongea katika kikao kilichofanyika Desemba 2, 2019 katika ofisi za Baraza la Wawakilishi. Kulia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Visiwani Zanzibar, Zubeir Ali Maulid.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Visiwani Zanzibar, Zubeir Ali Maulid amemueleza Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu kuwa kazi aliyopewa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ni kubwa na ngumu.

Spika Maulid alieleza hayo katika kikao kilichofanyika kwenye  ofisi za Baraza la wawakilishi  mapema leo (Desemba 2, 2019) alipotembelewa na Mwenyekiti huyo.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Augustino Mahiga baadhi ya machapisho kutoka tume katika kikao kifupi kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria.

Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustino Mahiga ameitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kuimarisha misingi ya utawala bora nchini ili kuboresha utoaji wa huduma za Serikali kwa jamii.

Waziri Mahiga alitoa kauli hiyo Novemba 18, 2019 jijini Dodoma katika kikao kilichofanyika kwenye ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria baina yake na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mheshimiwa Mathew Mwaimu.

Mwenyekiti wa (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu akiongea na wafanyakazi wa tume pamoja na wageni wengine waliohudhuria hafla fupi.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu ametembelea ofisi za taasisi hiyo zilizopo visiwani Zanzibar, ikiwa mara yake ya kwanza tangu alipokabidhiwa  dhamana hiyo Novemba 4, 2019.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu akiongea na waandishi wa habari mara baada kikao kifupi na watumishi wa tume kilichofanyika jijini Dodoma Novemba 11,2019.

Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amewasihi watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kutobweteka na elimu ambayo tayari wanayo na badala yake wafanye jitihada za kujiendeleza pale inapobidi kufanya hivyo.

Mwenyekiti huyo mpya wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora alitoa kauli hiyo katika hafla fupi ya kuwakaribisha viongozi wateule katika ofisi za makao makuu ya tume zilizopo jijini Dodoma Novemba 11, 2019.

Marehemu Getrude Alex pichani enzi za uhai wake

Getrude Alex (40), Afisa wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora amefariki dunia usiku wa Novemba 23, 2019 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Marehemu alikutwa na umauti baada ya kupata ajali ya kugongwa na pikipiki Novemba 21, 2019 katika eneo la ubungo jijini Dar es Salaam na kukimbizwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu an Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu akiongea na watumishi wa tume (hawapo pichani) katika hafla fupi iliyoandaliwa na Tume kuwakaribisha viongozi hao. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mheshimiwa Mohamed Khamis. Kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume, Hajjat Fatuma Muya na Kamishna, Mheshimiwa Khatib Mwinyi Chande.

Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amewasihi watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kutobweteka na elimu ambayo tayari wanayo na badala yake wafanye jitihada za kujiendeleza pale inapobidi kufanya hivyo.

Mwenyekiti huyo mpya wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora alitoa kauli hiyo katika hafla fupi ya kuwakaribisha viongozi wateule katika ofisi za makao makuu ya tume zilizopo jijini Dodoma Novemba 11, 2019.

Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (kulia) akimkaribisha Kamishna Rose Macharia kutoka Kenya alipofanya ziara katika ofisi za tume jijini Dodoma Novemba 22, 2019.

Kamishna wa Tume ya Maadili na Kupambana na Rushwa nchini  Kenya, Rose  Macharia ameikaribisha Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora (THBUB) kushirikiana  nao kufundisha elimu ya maadili ya viongozi katika chuo chao cha taifa cha maadili ili kukuza na kuimarisha utawala bora katika nchi hizo.

Macharia alitoa kauli hiyo katika ziara fupi aliyoifanya katika ofizi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora zilizopo Dodoma Novemba 22, 2019.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu (katikati-waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wateule wenzake. Kulia ni Makamu Mwenyekiti, Mheshimiwa Mohamed Khamis Hamad, Kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji, Hajjat Fatuma Muya. Wengine waliosimama kutoka kushoto ni Mheshimiwa Nyanda Josiah Shuli, Mheshimiwa Khatib Mwinyi Chande, Mheshimiwa Thomas Masanja, Mheshimiwa Amina Talib Ali na Dkt. Fatma Rashid Khalfan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli amemteua Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu kuwa Mwenyekiti  wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB).

Jaji Mwaimu aliteuliwa Oktoba, 2019 na kuapishwa rasmi Novemba 4, 2019 katika hafla  fupi ya kuapisha viongozi wateule iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai akiongea na viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (hawapo pichani) walipotembelea ofisini kwake Wilayani Kongwa Novemba 19, 2019. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa , Deogratius Ndejembi.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai ameihakikishia Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kuwa itaipatia kila aina ya ushirikiano itakayohitaji kutoka kwa taasisi ya Bunge.

Ndugai alieleza hayo mapema leo (Novemba, 19, 2019) alipokutana na Mwenyekiti wa Tume, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu aliyemtembelea katika ofisi yake ya jimbo iliyopo Wilayani Kongwa jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Mipango kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Laurent Burilo akiongea na washiriki wa kikao kazi cha kujadili hali ya haki za binadamu na kuibua matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu kwenye makundi ya wanawake, watoto na watu wenye ulemavu kilichofanyika Mkoani Morogoro, Oktoba 24—25, 2019.

Wadau wa haki za binadamu wameiomba Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora  kudumisha ushirikiano wa karibu na wadau wa taasisi zote ikiwemo za Serikali na Asasi za Kiraia ili kuendelea kujenga jamii  inayoheshimu na kuzingatia  haki za binadamu nchini.

More Articles ...

Sign up via our free email subscription service to receive notifications when new information is available.