22
Thu, Oct
1 New Articles

THBUB yahamia Dodoma

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inapenda kuujulisha umma wa Watanzania na wadau wake wote kuwa Makao Makuu ya ofisi yamehamia  jijini Dodoma.

Makao Makuu ya ofisi hiyo ambayo awali yalikuwa jijini Dar es salaam yamehamia jijini Dodoma rasmi mwezi Agosti, 2019. 

Kwa sasa Tume ipo Mtaa wa Kilimani na inapatikana  kwa anuani  ifuatayo:

Katibu Mtendaji,

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,

Mtaa wa Kilimani,

S.L.P 1049,

DODOMA.

Barua pepe ni This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. na Tovuti ni www.chragg.go.tz .

 

Aidha, Tume inapenda kuujulisha umma kuwa  kando na ofisi hizo za Makao Makuu zilizopo Mtaa wa Kilimani,ofisi zake nyingine zipo  Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) katika jengo la Wizara ya Katiba na Sheria ghorofa ya kwanza na ya pili.

Hivyo, Tume inatumia fursa hii kuwakaribisha wananchi na wadau wote kufika katika ofisi hizo au kutumia mawasiliano yaliyoandikwa  hapo juu ili kupata huduma.  

 

Bi.Madenge afungua mafunzo ya Watendaji wa Kata kuhusu haki za Binadamu,yaliyofanyika katika mkoa wa Lindi Julai 8, 2019.

Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Rehema Madenge amewataka Watendaji wa kata katika wilaya za Mkoa wa Lindi kusimamia haki za binadamu na upatikanaji wa haki kisheria.

Madenge alitoa wito huo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa watendaji wa kata kuhusu haki za binadamu na upatikanaji haki kisheria yaliyofanyika katika mkoa wa Lindi Julai 8, 2019.

Mkurugenzi wa Sheria kutoka taasisi ya Sheria Kiganjani, Jumanne Nabir (kulia) akimuonesha Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Alexander S. Hassan (katikati) namna ya mfumo wa sheria kiganjani unavyofanya kazi. Kushoto anayeangalia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria kutoka Tume, Nabor Assey.

Ujumbe wa taasisi ya Sheria Kigangani  umeitembelea Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora(THBUB) machi, 12, 2019.

Akiongea katika kikao  kifupi baina ya taasisi hizo,  Mkuu wa msafara huo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria wa taasisi hiyo ya Sheria Kiganjani, Jumanne Nabir  alisema kuwa lengo la ziara yao ni kujieleza na kujitambulisha kwa tume na kuona uwezekano wa kuanzisha ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili.

“Lengo la ujio wetu kwenu ni kujitambulisha  ili muijue  Sheria Kiganjani, namna inavyofanya kazi na faida zake kwa jamii na kuona uwezekano wa kushirikiana nanyi” alisema Nabir

Nabir aliendelea kueleza kuwa  sheria kiganjani ni mfumo unaomuwezesha mtu kupata huduma za kisheria kupitia simu yake ya mkononi.

“Mtu anaweza kupata huduma hii kupitia simu aina zote, simu za kawaida na smartpone, kwa sasa tupo katika utafiti na tangu tumeanza kazi mwaka jana mpaka sasa wamepatikana watumiaji elfu arobaini na tano (45,000) " aliongeza Nabir

Mkurugenzi huyo wa Sheria aliendelea kusema kuwa kupitia mfumo huo mwananchi anapata fursa ya kuunganishwa na mawakili kupitia simu yake popote nchini.

Kwa upande wa tume, Kaimu Katibu Mtendaji, Alexander S. Hassan aliipongeza taasisi hiyo kwa kuwa na ubunifu huo wa kuwasaidia  na kuwarahisishia watanzania kujua na kupata msaada wa sheria. 

Pia, aliuambia ujumbe huo kuwa tume inapata changamoto katika maeneo mawili ambayo ni namna ya kujitangaza na kutambulika kwa wananchi na pili ni namna ya kupata malalamiko yanayohusu uvunjwaji wa haki za binadamu nchini.

Kufuatia ujio wao, Hassan aliwaeleza kuwa tume inaona uwezekano wa kufanya kazi na Sheria Kiganjani upo, hivyo aliwataka wakamilishe taratibu za kuomba ushirikiano na tume ili kuwezesha kuanza kwa ushirikiano huo.

Ujumbe wa taasisi ya Sheria Kiganjani ulijumuisha watu wane (4) ambao ni Mkuu wa msafara, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria, Jumanne Nabir, Afisa Masoko, Brian Mallya, Afisa mifumo ya kompyuta, Mussa Kisena na Meneja Mradi, Chris Bwemo.

Sheria Kiganjani ni taasisi iliyoanzishwa na vijana wa kitanzania mwaka 2018 ambayo imetengeneza mfumo unaomuwezesha mwananchi wa kawaida kupata huduma za kisheria kupitia zimu yake ya mkononi, tovuti na mfumo wa  sms.

Mwisho.

THBUB yakutana na Wadau kubuni mbinu za kuelimisha jamii

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kuwashirikisha wadau wake kutoka taasisi za Serikali, Asasi za Kiraia na Vyombo vya habari wamekutana katika kikao kazi cha kubuni mbinu mbalimbali zinazolenga kuongeza uelewa kuhusu haki na haki za binadamu, hususan haki za wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.

Picha hapo juu ni Bw. Stanley Kalokola wakati akiwaelekeza Wasaidizi wa Kisheria namna ya kutuma malalamiko THBUB kwa kutumia njia ya ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani (SMS) wakati mafunzo yaliyofanyika Kituo cha wasaidizi wa kisheria kilichopo Momba mkoani Songwe.

Wasaidizi wa sheria (paralegals) waliopo Halmashauri ya Mji wa Tunduma mkoani Songwe  wameelimishwa namna ya kuwasilisha lalamiko Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora  kupitia simu ya kiganjani.

Wasaidizi hao wa kisheria wapatao kumi na mbili (12) walipata elimu hiyo katika warsha iliyoandaliwa na Tume Februari, 21-22, 2019 katika ofisi za kituo cha wasaidizi wa sheria kilichopo Momba, Halmashauri ya Mji wa Tunduma, Mkoani Songwe.

Akiongea katika warsha hiyo, Muwezeshaji, Afisa Uchunguzi wa Tume, Stanley Kalokola alisema kuwa Tume imeanzisha mfumo huu wa kuwasilisha lalamiko kupitia simu ya kiganjani ili kuwarahisishia wananchi na kuwapunguzia gharama na kuokoa muda.

Kalokola aliendelea kuwaeleza wasaidizi hao kuwa mfumo huo wa mawasiliano ni kwa njia ya meseji tu na haipaswi kupiga kwani haitapokelewa.

“Mwananchi mwenye lalamiko lake au taarifa kuhusu uvunjwaji wa haki za binadamu au ukiukwaji wa misingi ya utawala bora anaweza kutuma ujumbe wa simu ya kiganjani kwenda namba 0737 446 787,” alisema Kalokola

Kalokola alifafanua kuwa kupitia utaratibu huo, mara baada ya lalamiko au taarifa kufika tume, Afisa wa Tume atakayelipokea anaweza kupiga simu kwa mlalamikaji ili kupata maelezo zaidi kabla ya kuanza kushughulikia lalamiko hilo.

Aidha, Kalokola aliwaeleza wasaidizi hao wa sheria kuwa ili lalamiko liweze kufika kwa usahihi, mwananchi anatakiwa kuandika lalamiko lake kwa ufupi na kulituma kwa kuanza na neno ‘REPORT’ kwenda 0737 446 787.

Mbali na kuwasilisha lalamiko kwa tume kupitia simu ya kiganjani, mlalamikaji anaweza pia kuwasilisha lalamiko lake kwa kufika katika ofisi za Tume au kuandika barua ya lalamiko lake na kuituma kwa njia ya Posta.

MWISHO.

Mratibu wa Mradi wa upatikanaji wa haki, Laurent Burilo akitoa mada kwa ufupi kuhusu mradi wa upatiakanaji wa haki katika kikao kazi cha kuandaa hadidu za rejea na muongozo kwa ajili ya makundi ya utetezi wa haki za binadamu kinachofanyika mkoani Morogoro kuanzia Juni 20-22, 2019.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kushirikiana na wadau wake wanaandaa hadidu za rejea na muongozo kwa ajili ya kuyawezesha makundi ya utetezi wa haki za binadamu kufanya kazi zake vizuri.

Akifungua kikao kazi cha kuandaa hadidu za rejea na muongozo kwa ajili ya makundi hayo ya haki za binadamu kinachofanyika mkoani Morogoro kuanzia Juni 20-22, 2019,   Mkurugenzi wa Idara ya Elimu kwa Umma na Mafunzo kutoka Tume, Alexander Hassan alisema kuwa hadidu za rejea na muongozo vitasaidia makundi hayo ya haki za binadamu kufanya kazi zake kwa wepesi.

Kaimu Katika Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Hajjat Fatuma I. Muya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi kilichofanyika feb. 5, 2019, 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), inategemea kuwa na ushirikiano wa kikazi baina yake na shirika la kimataifa lijulikanalo kwa jina la National Democratic Institute (NDI). 

Hayo yalisemwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa THBUB Hajat Bibi Fatuma I. Muya kwenye kikao kazi kilichohusisha baadhi ya watumishi wa Tume na Maafisa watatu (3) kutoka shirika la NDI. 

Akiongea kwenye kikao hicho Afisa wa NDI Bi. Juliana Brother alisema shirika la NDI llinalenga kushirikiana na Tume kwenye masuala ya Haki za Binadamu na utawala bora.

Pamoja na kueleza majukumu ya Tume Bibi. Fatuma pia aliwashukuru maafisa wa NDI kwa kuwa tayari kutanya kazi na Tume, hasa katika masuala ya haki za binadamu na utawala bora.

Kikao kazi hicho kilichofanyika tarehe  5 Februari, 2019 katika ofisi za Makao Makuu ya Tume Jijini Dar es salaam kilihusisha pia baadhi ya maafisa wa Tume kutoka Idara ya Sheria, Utawala Bora na  Haki za Binadamu.

Washiriki wengine ni Bi. Sarolly Quibaya na Bi. Mahiga Dodd  wote kutoka shirika la NDI.

 

 

Bw. Victor Rugarabamu, Mwezeshaji kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (WAMJJW), akizungumzia masuala ya mahusiano kati ya Serikali na Asasi za Kiraia (AZAKI)kwenye mkutano uliofanyika tarehe 17-19 Juni, 2019, katika ukumbi wa Cherry Hotel Mjini Morogoro, uliolenga kufanyia tathimini mafanikio, changamoto na matarajio ya makubaliano hayo.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imekutana na Asasi za Kiraia (AZAKI) ilizoingia nazo makubaliano ya kushirikiana kwa lengo la   kujifunza, kubadilishana uzoefu na mawazo ya namna ambavyo taasisi hizo zitakuwa na ushirikiano wenye tija katika utekelezaji wa kazi zao za kila siku.

Akifungua mkutano huo Juni 17, 2019 Mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa Idara ya Elimu kwa Umma na Mafunzo, Alexander Hassan ambaye alimuwakilisha Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora alisema kuwa 

Ni ukweli usiopingika kuwa bila mashirikiano yenye tija miongoni mwa tume  na AZAKI matokeo ya kazi zao hayatawezi kuwa makubwa.

Hivyo mkutano huo umelenga katika kuboresha ushirikiano huo ili uwe na manufaa kwa jamii wanayoihudumia.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Hajjat Fatuma Muya akiongea na wajumbe wa mkutano wa kumi na saba (17) wa baraza la wafanyakazi (hawapo pichani) alipokuwa akifungua mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam Januari 23, 2019. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Elimu kwa Umma na Mafunzo wa Tume, Alexander S. Hassan.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Hajjat Fatuma Muya amewataka wafanyakazi wa taasisi hiyo kuzingatia haki na wajibu wakati wanatekeleza majukumu yao.

Na Getrude Alex

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), hivi karibuni ilifanya kikao kazi na mwakilishi wa Asasi ya Kiraia ijulikanayo kwa jina la “CEFA” (Comitato Europeo per la Formazione el’ Agricoltura Onlus)  

Mazungumzo hayo ya siku moja yalilenga kujenga mashirikiano ya kikazi, baina ya THBUB na shirika la CEFA hususani kwenye suala la kukomesha ukatiri  na mauaji kwa  watoto na watu wenye ulemavu wa Ngozi.

Afisa Uchunguzi Mkuu wa THBUB na Kaimu MKuu wa Kitengo cha Mipango, Bw. Laurent Burilo akitoa ufafanuzi juu ya malengo ya mafunzo kwa watendaji wa kata katika masuala ya haki za binadamu na upatikanaji wa haki kisheria, yaliyofanyika Januari 8-9, 2019, katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora  (THBUB) kwa  ufadhiri wa Asasi ya Kiraia ijulikanayo kwa jina la “Legal Service Facility” (LSF), hivi karibuni imefanikiwa  kutoa mafunzo ya elimu ya haki za binadamu na upatikanaji  wa haki kisheria kwa watendaji  kata  wapatao 128 kutoka kata sita (6) za Mkoa wa  Shinyanga.

More Articles ...

Sign up via our free email subscription service to receive notifications when new information is available.