ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB NA ARUMERU DC KUSHIRIKIANA KUPINGA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO.

28 Oct, 2026
THBUB NA ARUMERU DC KUSHIRIKIANA KUPINGA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO.

 

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Neema Lugangira ameahidi ushirikiano kati ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) na uongozi wa wilaya hiyo katika kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwenye kikao kilichofanyika Oktoba 23, 2026 katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wakati THBUB  ilipofika kwa lengo  la kujadili masuala ya haki za binadamu.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Lugangira ameeleza umuhimu wa kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu haki za binadamu, kuhamasisha jamii kutoa taarifa za vitendo vya ukatili na kuhakikisha kuwa hatua stahiki zinachukuliwa kwa mujibu wa sheria dhidi ya wahusika wa vitendo hivyo.

"Mapambano dhidi ya ukatili yanahitaji ushiriki wa viongozi wa Serikali, vyombo vya ulinzi na usalama, taasisi zinazohusika na ustawi wa jamii, asasi za kiraia pamoja na wananchi kwa ujumla ili kuzuia vitendo hivyo na kuhakikisha waathirika wanapata msaada unaostahili", amesema Mhe. Lugangira.

Naye Kaimu Mkurugenzi  Msaidizi Utafiti na Nyaraka  wa THBUB, Bw. Paul Sulle ameeleza kuwa THBUB inashirikiana na viongozi wa Serikali na asasi  za kiraia  katika kuelimisha wananchi kuhusu haki za binadamu na utawala bora, kupokea na kushughulikia malalamiko yanayohusu ubunjifu wa haki hizo na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.

Bw. Sulle amesema kuwa THBUB inaendelea kuhimiza ushirikiano na wadau mbalimbali katika kuendeleza uelewa wa wananchi kuhusu haki za binadamu na misingi ya utawala bora  pamoja na kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuhakikisha kuwa haki zao zinalindwa na kuheshimiwa.

Ushirikiano kati ya THBUB na Wilaya ya Arumeru unalenga kuongeza juhudi za kuimarisha ulinzi wa haki za binadamu na kuhamasisha jamii kushiriki katika kupinga ukatili, ili kujenga jamii yenye amani, usawa na ustawi kwa wote.

slot gacor