ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YAADHIMISHA WIKI YA MAZINGIRA KWA KUZINDUA BUSTANI YA MITI JIJINI DODOMA.

04 Jun, 2026
THBUB YAADHIMISHA WIKI YA MAZINGIRA KWA KUZINDUA BUSTANI YA MITI JIJINI DODOMA.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) leo tarehe 04 Juni, 2026 imezindua bustani ya miti katika Mtaa wa Salama, Kata ya Nkuhungu, Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Mazingira.

Akizungumza katika hafla hiyo kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Nkasori Sarakikya, amesema kuwa haki za binadamu na mazingira ni mambo yanayohusiana moja kwa moja na hayawezi kutenganishwa.

“Kulinda mazingira ni kulinda haki za binadamu, na kulinda haki za binadamu yapasa kuendana na kuhifadhi mazingira,” amesema Bi. Sarakikya. Pia alisisitiza kuwa mazingira safi, salama na endelevu ni haki ya msingi ya binadamu inayotambulika kitaifa na kimataifa.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa THBUB, Bw. Patience Ntwina amesema uzinduzi wa bustani hiyo unaonesha kwa vitendo namna Tume inavyotekeleza jukumu lake la kuhamasisha hifadhi ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora kupitia shughuli za utunzaji wa mazingira.

Bw. Ntwina amesema, “tunayo furaha kubwa sana siku ya leo, si kwa sababu ya bustani pekee, bali kwa sababu shughuli hii inaonesha namna haki za binadamu zinavyofungamana na mazingira tunayoyaishi kila siku.” Ameongeza pia, bustani hiyo ni sehemu ya juhudi za Tume za kuchangia ustawi wa jamii na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa eneo hilo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Salama, Bw. Habasi Mwijuki amesema bustani hiyo imebadilisha kabisa sura ya eneo ambalo hapo awali lilikuwa kame na lisilovutia.

Uzinduzi wa bustani hiyo ni sehemu ya matukio kuelekea kilele cha Siku ya Mazingira Duniani ambayo huadhimishwa Juni 5 kila mwaka.

slot gacor