ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YAFIKISHA ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU JUKWA LA TATU LA VYAMA VYA USHIRIKA WA MAENDELEO.

07 May, 2026
THBUB YAFIKISHA ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU JUKWA LA TATU LA VYAMA VYA USHIRIKA WA MAENDELEO.

Afisa Mchunguzi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Tawi la Tabora, Bw. Raphael Mavunde, ametoa elimu kuhusu Haki za Binadamu na Misingi ya Utawala Bora katika Jukwaa la Tatu Vyama vya Ushirika wa Maendeleo lililofanyika Wilayani Kaliua, Mkoa wa Tabora. Mafunzo hayo yalilenga kuongeza uelewa wa washiriki kuhusu umuhimu wa kuheshimu haki za binadamu pamoja na kuzingatia misingi ya uongozi bora katika shughuli za maendeleo.

Jukwaa hilo lililodumu kwa siku mbili kuanzia tarehe 29 hadi 30 Aprili, 2026, limekuwa fursa muhimu ya kujadili mchango wa vyama vya ushirika katika maendeleo ya jamii. THBUB imeendelea kusisitiza kuwa ulinzi wa haki za binadamu na utawala bora ni nguzo muhimu katika kujenga jamii yenye usawa, uwajibikaji na maendeleo endelevu.

slot gacor