WAKAZI WA DODOMA NA MIKOA JIRANI WAFIKA BANDA LA THBUB MAONESHO YA NANENANE

Wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa Jirani wanaendelea kufika katika Banda la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kufahamu haki zao na wajibu katika kulinda na kukuza haki za binadamu nchi ni.
Akizungumza na wananchi waliotembelea Banda la THBUB Afisa Uchunguzi Mkuu Msaidiizi Bw. Halfan Botea amesema kuwa haki za binadamu ni za kila mtu ,kila mahali kwasababu ya kuwa ni binadamu.Zinavuka mipaka ya rangi, jinsia,taifa na Imani,zinahakikisha usawa na heshima ya asili kwa wote.
"Haki hizi binadamu huzaliwa nazo na kila mtu anatakiwa kuzipata"amesema Bw.Botea
Pia Bw.Botea ameweleza wananchi hao kuwa haki za binadamu haziwezi kuondolewa au kubatilishwa,isipokuwa
katika hali maalum za kisheria,kama vile kufungwa kwa kufuata utaratibu unaostahili.
Aidha,Bw.Botea ameeleza wajibu wa kila mtu katika kupata haki kupata.
“haki inaendana na wajibu ,kila mtu anahaki ila haki hizo lazima ziendane na wajibu’amesema Bw.Botea
Kwa upande wake Rahimu Juma Mkazi wa Dodoma ametoa shukrani kwa THBUB kutoa elimu hiyo
"Elimu niliyopata leo ni msaada kwa wengine kujua haki zao"amesema Bw.Juma
Maadhimisho ya Maonesho Nanenane Kitaifa yamefunguliwa Agosti 2 ,2025 na Makamu wa Rais Dkt.Isdory Philip Mpango katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.