ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

WANAFUNZI  WAPATIWA ELIMU YA HAKI  ZA BINADAMU 

11 Aug, 2025
WANAFUNZI  WAPATIWA ELIMU YA HAKI  ZA BINADAMU 

 

Haki za binadamu  zinaendana na wajibu,

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Uchunguzi Mkuu Bw. Fadhili Muganyizi wakati akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari  St Gabriel Tech walipotembelea Banda Tume ya Haki za Binadamu   Utawala Bora katika Maonesho ya Kitaifa ya Nane Nane yanayofanyika katika Viwanja vya  Nzuguni Jijini Dodoma.

Bw. Muganyizi amesema kuwa watoto wana haki ya kuishi, kusikilizwa, kutoa maoni, kupata taarifa na haki ya kupata elimu

"Haki zote ni muhimu kuzipata na THBUB  pia ina jukumu la kutoa elimu kwenu ili muweze kuzijua" amesema Bw. Muganyizi

Pia Bw. Muganyizi amewaeleza wanafunzi hao kuhusu wajibu wao wanapokuwa shuleni na katika Jamii kwani wao ni viongozi wa baadae.

"Pamoja na kuwa na haki ya kupata elimu, pia mna wajibu wa kusoma ili muweze kufaulu sambamba na kuheshimu jamii inayowazunguka ili kuwa viongozi bora wa  baadae" amesema Bw. Muganyizia 

Aidha, wanafunzi hao walielezwa pia majukumu ya THBUB ambapo pia walipata fursa ya kuuliza maswali kuhusu haki za binadamu  na utawala bora .

Kwa wapande wake Anthonia Vendeline Mwanafunzi wa Kidato cha Nne kutoka Shule hiyo  ameishukuru THBUB  kwa kuwapatia elimu hiyo  ambayo imewasaidia kutambua haki na wajibu wao sambamba na kuijua THBUB. 

"Tumefurahi, asanteni sana" amesema Anthonia