ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

WATUMISHI THBUB WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

23 Jun, 2025
WATUMISHI THBUB WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria,Dkt Franklin Jasson Rwezimula ametoa wito kwa Watumishi  Tume ya Haki na Utawala Bora kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ili wapate haki zao.

Dkt Rwezimula ametoa wito huo  Juni 23,2023 wakati alipotembelea Banda la THBUB  katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.

Dkt.amesema kuwa wananchi wanapopata changamoto ya haki za binadamu na utawala bora wanaamini kuwa hapa ni mahala sahihi kwa kupata haki zao

“Hivyo nanyi mshughulikie malalamiko yao kwa  ueledi na ufanisi ili wapate haki zao”amesema Dkt. Rwezimula


Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yalifunguliwa Juni 16,2025 ikiwa na  lengo kuwahudumia Watumishi wa Umma na Wananchi kwa pamoja.