ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

WIZARA YA KILIMO KUSHIRIKIANA NA THBUB. 

11 Aug, 2025
WIZARA YA KILIMO KUSHIRIKIANA NA THBUB. 

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Athuman Kilundunya amesema kuwa Wizara ya Kilimo ipo tayari kushirikiana na Tume ya Haki za Binadamu  na Utawala katika ulinzi wa haki za binadamu haswa haki ya kuishi katika jamii zenye migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Mhandisi Kilundunya ameyasema hayo Agosti 4,2025 wakati alipotembelea banda la THBUB  katika Maonesho  ya Nanenane   Viwanja vya Nzuguni Jijini  Dodoma.
Mhandisi  Kilundunya ameeleza  kuwa kati ya mambo ambayo Wizara ya Kilimo inapambana nayo ni migogoro iliyopo  katika baadhi ya maeneo  ya Wafugaji na Wakulima  ambapo kuna wakati hupelelekea kuvunjwa kwa haki za binadamu ikiwemo haki ya kuishi.
"Tushirikiane katika kutatua migogoro, THBUB mnaweza kutuletea ushauri kutokana na chunguzi mnazozifanya zinazohusu masuala ya wakulima na wafugaji tusaidie ndugu zetu " Alisema
Naye Mkurugenzi  Msaidizi Elimu kwa Umma na Mawasiliano Tume ya Haki za Binadamu  na Utawala Bora Bi.Zawadi Msalla amesema Wizara ya Kilimo ni kati ya wadau  muhimu wa  THBUB. 
 "Tumekuwa na ushirikiano wa karibu na Wizara ya Kilimo na tunaahidi kuendelea kushirikiana katika usimamizi wa haki za binadamu” Alisema
 
Aidha, Bi. Zawadi alieleza kuwa THBUB  imeshiriki katika maonesho ya Nanenane ili kutoa elimu,ushauri wa kisheria pamoja na kupokea malalamiko ya uvunjifu wa haki za binadamu na utawala bora.