SHULE SITA, LENGO MOJA: KUJENGA UTAMADUNI WA HAKI NA WAJIBU KUPITIA KLABU ZA HAKI ZA BINADAMU
Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Tawi la Mwanza, wametembelea shule sita zenye Klabu za Haki za Binadamu Jijini Mwanza kwa lengo la kujadili namna bora ya kuendeleza shughuli za klabu hizo katika kukuza uelewa wa wanafunzi kuhusu haki za binadamu na misingi ya utawala bora.
Katika ziara hiyo, watumishi hao walioongozwa na Afisa Uchunguzi Mkuu, Bw. Chrisantus Ndibaiukao walikuwa na walimu wakuu wa shule husika na kuzungumzia umuhimu wa klabu hizo katika kuwajengea wanafunzi uelewa kuhusu haki zao, wajibu wao, kuheshimu haki za wengine na kushiriki katika kujenga mazingira salama na yenye uwajibikaji shuleni.
Aidha, Tume imekabidhi vifaa vya uhamasishaji na nyenzo za kuwezesha shughuli za klabu, zikiwemo vikombe vyenye nembo na kauli mbiu , “Haki Zetu, Wajibu Wetu, Sauti Zetu,” pamoja na shajara na vitabu vya kumbukumbu za shughuli .
Vifaa hivyo vimetolewa kwa lengo la kuwasaidia walimu walezi wa klabu katika shule husika kuratibu, kurekodi na kuendeleza shughuli za klabu.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Afisa Uchunguzi Mkuu, Bw. Chrisantus Ndibaiuka amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Tume na uongozi wa shule katika kuendeleza klabu hizo.
“Klabu za haki za binadamu ni jukwaa muhimu la kuwasaidia wanafunzi kujifunza haki zao na wajibu wao tangu wakiwa shuleni. Ushirikiano wa walimu wakuu na walimu walezi ni muhimu ili klabu ziweze kutekeleza shughuli zake na kuendeleza utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu.”
Kwa upande wake Mwl. Anthony Mtokambali, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Buhongwa amesema kuwa ushirikiano na Tume pamoja na nyenzo zilizotolewa utasaidia walimu walezi kupanga na kufuatilia shughuli za klabu
“Tunathamini ushirikiano wa Tume na shule yetu. Vifaa hivi vitawasaidia walimu walezi kuratibu na kutunza kumbukumbu za shughuli za klabu, huku wanafunzi wakipata nafasi zaidi ya kujifunza kuhusu haki na wajibu wao.”
THBUB imeendelea kuimarisha mawasiliano kati yake na shule zenye klabu za haki za binadamu ili kuwajengea wanafunzi uelewa kuhusu haki za binadamu na utawala bor

