ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB IMEPOKEA MALALAMIKO 41 YA UVUNJIFU WA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA.

28 Oct, 2026
THBUB IMEPOKEA MALALAMIKO 41 YA UVUNJIFU WA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA.

 

Naibu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bw. Juma Msafiri Karibona, amesema kuwa jumla ya malalamiko 41 yanayohusu madai ya uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora yamepokelewa Tume, ofisi ya Zanzibar kwa kipindi cha miezi Aprili hadi Septemba, 2026.

Bw. Karibona ameyasema hayo, alipozungumza katika Kipindi cha "Nahodha" kinachorushwa na redio ya Bahari FM iliopo Migombani, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Oktoba 26, 2026.

Akiainisha aina ya malalamikao ambayo yaliyopokelewa, Bw. Karibona amesema malalamiko hayo ni pamoja na madai ya umiliki wa mali zilizoathiriwa na changamoto zilisosababishwa na ujenzi wa miradi ya maendeleo ikiwemo miradi ya ujenzi na upanuzi wa barababra ulioathiri maeneo mengi ya mji wa Zanzibar.

Malalamiko mengine ameeleza yalihusu madai ya wastaafu waliokuwa utumishi wa umma.

Aidha, Bw. Karibona amesema THBUB kwa kuzingatia sheria imeendeleea kushirikiana na taasisi zinazolalamikiwa kushughulikia malalamiko hayo.

Katika hatua nyingine, Bw. Karibona ametoa wito kwa jamii, viongozi wa dini na Serikali kushirikiana pamoja katika kuhubiri amani ya nchi na kuendelea kuuelimisha umma juu ya kuheshimu haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

"Wito wetu na ujumbe wetu kwa jamii, tujenge jamii yenye kuheshimu haki za binadamu, kutii utu wa mtu bila ya ubaguzi wowote ili kupata jamii iliyo bora". amesisitiza Bw. Karibona.

slot gacor