ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

UTEUZI WA MWENYEKITI NA MAKAMU MWENYEKITI WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

28 Oct, 2026
UTEUZI WA MWENYEKITI NA MAKAMU MWENYEKITI WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Leo Oktoba 28, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Kasiluka, Bw. Dunford George Mpelumbe ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) na Bw. Omar Ali Omar ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mpelumbe alikuwa Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu Pauwa Maimu ambaye amemaliza muda wake.

Aidha, kabla ya uteuzi huo, Bw. Omar alikuwa Mkuu wa Idara ya Utawala ,Mipango na Fedha katika Taasisi ya sayansi na Technolojia Karume Zanzibar na anachukua nafasi ya Bw. Mohamed Khamis ambaye amemaliza muda wake.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa uapisho wa viongozi wateule utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

slot gacor