ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

MHE. AMINA TALIB ALI

AMINA TALIB ALI photo
MHE. AMINA TALIB ALI
Kamishna

Barua pepe: amina.ali@chragg.go.tz

Simu: 0734047775

Wasifu

Mhe. Amina Talib Ali, Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kuanzia Septemba 19, 2019. Kabla ya hapo alikuwa Mratibu wa Shughuli za Muungano, Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera Uratibu na Shughuli za Baraza la Wawakilishi, Zanzibar 2008 hadi 2014.

Pia, alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia iitwayo Zanzibar Female Lawyers Association (ZAFELA) inayoshughulikia haki za wanawake na watoto kwa kipindi cha miaka sita (2010 hadi 2015).

Kitaaluma ni mwanasheria na mwalimu aliyefundisha katika skuli mbalimbali huko Zanzibar kwa takriban miaka 15.