Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi.Mary Makondo akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya siku 10 za kupinga ukatili dhidi ya watoto uliofanyika Juni6,2022 katika ofisi za Tume zilizopo Mtaa wa Kilimani Jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw.Patience Ntwina akitoa utambulisho wa awali kwa waliohudhuria Uzinduzi wa siku 10 za kampeni ya Kupinga ukatili dhidi Watoto uliofanyika katika Ofisi za Tume zilizopo Mtaa wa Kilimani Dodoma Juni6,2022.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe.Mohamed Hamisi akizunguza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku 10 za kupinga ukatili dhidi ya watoto uliofanyika katika Ofisi za Tume zilizopo Mtaa wa Kilimani Jijini Dodoma Juni 6,2022.
Mkaguzi wa Polisi Mkoa wa Dodoma Christer Kayombo anayeshughulikia Dawati la Jinsia akiiongoza maandamano ya uzinduzi wa siku 10 za kupinga ukatili dhidi ya watoto Juni 6,2022 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi.Mary Makondo (katikati)Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Katibu Mtendaji,Watumishi na Wadau wengine wakiwa katika katika maandamano ya Uzinduzi wa kampeni ya siku 10 za kupinga ukatili dhidi ya Watoto yaliyoanzia Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodom hadii Ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Juni 6,2022.
Baadhi ya Wanafunzi wakiwa wameshikilia mabango yenye jumbe mbalimbali zinazoeleza namna ya kuwalinda na kutetea haki za watoto wakati wa maandamano yaliyoandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Juni 6,2022 Jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Patience Ntwina(Kulia) akizungumza na Uongozi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu alipotembelea Ofisi za Kituo hicho kwa lengo la kujitambulisha na kuendeleza mashirikiano Mei 12,2022 Kijitonyama Dar es Salaam
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw.Patience Ntwina(wa kwanza kushoto) alipotembelea Shirika linalotoa huduma za kisheria(LSF) na kupokelewa na Bi.Lulu Ngwanakilala (wa Nne kulia) kwa lengo la kujitambulisha na kujadili namna ambavyo shirika hilo litaendelea kushirikiana na Tume katika kufanya kazi za kulinda na kutetea Haki za Binadamu Mei 18,2022 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw.Patience Ntwina(Kushoto) akipokea kitabu chenye taarifa za Mwaka kuhusu maswala ya Haki za Binadamu kutoka kwa Mkurugenzi wa Haki Maendeleo Bw.Wilfred Warioba Katika ofisi za Taasisi hiyo zilizopo sinza ,Dar es Salaam.