Kitengo cha Mipango na Bajeti
Majukumu ya Kitengo
i. Kuratibu mchakato wa maandalizi na utekelezaji wa mipango na bajeti ya shughuli za Tume
ii. Kuratibu uandaaji wa mpango kazi wa mwakana mpango mkakati wa Tume;
iii. Kuainisha miradi ,programu,mipango kazi na kuendeleza mikakati ya ukusanyaji wa rasilimali;
iii. Kuratibu maandalizi ya maandiko ya miradi na programu kwa ajili ya kupata rasilimali fedha za ndani na nje ya nchi;
iv. Kuratibu ukusanyaji, uchambuzi, tafsiri na uwasilishaji wa takwimu za Tume;
v. Kuratibu mapitio ya nusu na mwaka ya utendaji kazi wa Tume ;
vi. Kuratibu uandaaji wa taarifa za wiki, mwezi, robo, nusu na mwaka za utekelezaji wa majukumu ya Tume; and
vii. Kufanya ufuatiliaji/utafiti wa maoni ya wadau kuhusu huduma zinazotolewa na Tume.

