ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Hon. Jaji Mst. MATHEW PAUWA MHINA MWAIMU

MATHEW PAUWA MHINA MWAIMU photo
Hon. Jaji Mst. MATHEW PAUWA MHINA MWAIMU
Mwenyekiti

Barua pepe: mathew.mwaimu@chragg.go.tz

Simu: 0734047775

Wasifu

 Jaji (Mst) Mathew Pauwa Mhina Mwaimu, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kuanzia tarehe 19 Septemba, 2019. 

Pia, alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kati ya mwaka 2012 na 2016.  Kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi wa Katiba na Haki za Binadamu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali’;Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria; Mjumbe wa mabaraza na bodi za taasisi mbalimbali nchini ikiwemo;- African Peer Review Mechanism, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Chuo cha Teknolojia (DIT) Dar es Salaam, Baraza la Kumbukumbu za Nyaraka pamoja na Baraza la Veterinari Tanzania kwa nyakati tofauti.

Kitaalamu ni Mwanasheria mbobezi  aliyehitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1989, lakini pia ni mhitimu wa Stashahada ya Ualimu kutoka kilichokuwa Chuo cha Ualimu Dar es Salaam mwaka 1982.

Pamoja na hayo pia amepata mafunzo ya muda mfupi ndani na nje ya nchi kuhusu haki za binadamu, uandishi wa taarifa kuhusu masuala ya haki za binadamu, masuala ya uongozi na uandaaji wa bajeti.