ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

MHE. NYANDA JOSIAH SHULI

NYANDA JOSIAH SHULI photo
MHE. NYANDA JOSIAH SHULI
Kamishna

Barua pepe: nyanda.shuli@chragg.go.tz

Simu: +255 764 600 170

Wasifu

Mhe. Nyanda J. Shuli, Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora tangu 19 Septemba 2019. Katika kipindi cha zaidi ya miaka 18 ya utumishi wangu, nimefanya kazi na taasisi mbalimbali katika za sekta ya umma na binafsi. Katika kipindi hiki, nimekuwa nikitumia maarifa niliyo nayo katika eneo la mawasiliano ya kimkakati katika kutetea na kukuza haki za kijamii, haki za binadamu, demokrasia, na maendeleo.

Pamoja na uzoefu nilio nao, nina Shahada ya Uzamili ya Mawasiliano (Master of Communication-MComn) kutoka The Hague University of Applied Sciences cha Uholanzi, ambayo niliipata mwaka 2009. Aidha, mimi ni mhitimu wa shahada ya kwanza ya Sanaa na Elimu (Bachelor of Arts with Education-BAED) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wa mwaka 2003. Katika kuongeza maarifa, nimeshiriki mafunzo mbalimbali yanayojumuisha mada kama vile Uandishi wa Habari wa Kiraia (Citizen Journalism), Matumizi ya Teknolojia katika Uchechemuzi (Use of Technology for Advocacy Interventions), na Usimamizi Wenye kuleta Matokeo (Results Based Management). Safari yangu ya kitaaluma na kikazi imechochea ari kubwa ya utafiti ndani yangu katika eneo la haki za kiuchumi, hususan kuhusu jamii za wenyeji wanaozunguka migodi mikubwa ya uchimbaji wa madini nchini Tanzania.

Nimewahi kupata heshima ya kuhudumu kama mjumbe wa Baraza la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano la Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania kuanzia mwaka 2015 hadi 2018.