THBUB KUSHIRIKIANA NA WADAU KATIKA KUSIMAMIA HAKI ZA WAVUVI WADOGO.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inmedhamiria kuhakikisha haki za binadamu zinaheshimiwa,kulindwa na kutekelezwa kwa usawa na haki katika nyanja zote za maisha,hii muhimu kwa makundi yanayokumbwa na changamoto mbalimbali wakiwemo wavuvi wadogo.
Hayo amesema Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw.Patience Ntwina wakati akifungua kikao cha kuwasilisha na kujadili rasimu ya taarifa ya uchambuzi wa awali kuhusu haki za wavuvi wadogo katika upatikanaji na usimamizi wa rasilimali za Bahari.
Bw.Ntwina amesema kuwa kikao cha ushirikishwaji wa wadau ni hatua inayolenga kuhakikisha kuwa maoni na uzoefu vinajumuishwa ili kuboresha rasimu ya taarifa husika.
‘’THBUB inatambua kuwa wavuvi wadogo ni Kundi lenye mchango mkubwa katika Uchumi wa taifa,ustawi wa jamii za pwani, na uhifadhi wa mazingira ya Bahari”.amesema Bw.Ntwina
Pia Bw.Ntwina amebainisha kuwa kupitia uchambuzi huo na majadaliano THBUB itatumia nyenzo thabiti ya kuishauri serikali na wadau wengine katika maboresho ya sera,sheria, miongozo na na taratibu zinazohusu usimamizi wa rasilimali za bahari zitakazosaidia kuleta mabadiliko Chanya yanayolinda maslahi ya wavuvi wadogo kwa manufaa ya sasa na vizazi viavyo.

