emblem

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu

Habari

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA YAADHIMISHA KILELE CHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA


Juni 23,2022 Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi Portacia Benito alifanya kikao na Watumishi na kuzungumza masuala mbalimbali ya kiutumishi ikiwemo mafanikio na changamoto za kiutendaji.

Katika kikao hicho aliwaasa watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria za utumishi wa Umma ikiwa ni pamoja na kuhudhuria kazini kwa wakati na kufanya kazi kwa bidii na maarifa.

Aidha Bi.Benito alisisitiza ushirikiano katika utendaji wa kazi kwa lengo la kuongeza tija katika utumishi wa Umma.

“Kila mtumishi awajibike kwa nafasi yake,inapotokea mtumishi anapata changamoto yeyote asisite kutoa taarifa”Alisema Bi.Benito

Akizungumza kwa niaba ya Watumishi wengine Bw.Yohana Tumaini Mcharo Mchunguzi Mkuu Msaidizi alipongeza Uongozi wa Tume kwakuwakutanisha watumishi pamoja na kusikiliza changamoyo zao,maoni na ushauri sambamba na kuipongeza Serikali kwakuendelea kusimamia maslahi ya Watumishi.

“Naamini kupitia kikao hiki hoja za Watumishi zitajibiwa na ambazo majibu yake si ya papo kwa papo naamini uongozi utayafanyia kazi”Alisema Bw.Mcharo

Kwa hatua nyingine Bi.Benito alipata nafasi kutoa majibu kwa baadhi ya hoja zilizowasilishwa na Watumishi na nyingine zisizopata majibu ya papo kwa papo aliahidi kuzipokea na kuzifanyia kazi.

Kikao hicho kilifanyika katikaOfisi za Makao Makuu ya Tume zilizopo eneo la Kilimani,Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Wakurugenzi wa Idara na Vitengo pamoja watumishi.