ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Juma M. Karibona

Juma M. Karibona photo
Juma M. Karibona
Katibu Mtendaji Msaidizi

Barua pepe: juma.karibona@chragg.go.tz

Simu:

Wasifu

Wasifu wa NKM

Wakili Mkuu wa Serikali Afisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Zanzibar kwa kipindi cha miaka tisa (9) na Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Kesi  za Madai akiwa na jukumu la kutoa maoni ya kisheria, kuandaa nyaraka za kisheria za utetezi, madai na kuiwakilisha Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mahakamani. Kabla ya kipindi hicho alihudumu kama Wakili wa Serikali katika Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar akishughulika na kutoa maoni ya kisheria, kuiwakilisha Serikali Mahakamani katika kesi za jinai na pia akisimamia na kuendesha kesi za jinai katika ngazi ya rufaa Mahakama Kuu Zanzibar na Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Akiwa katika Utumishi wa Umma Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika nyakati tofauti ametumikia kwa kuazimwa katika Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa muda wa mwaka mmoja akihudumu katika kitengo cha sheria.

Kwa sasa ni Katibu Mtendaji Msaidizi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora akiwa na jukumu la kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Tume kwa ujumla katika Afisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Zanzibar.

Vile vile, sambamba na nafasi hii ni Kamishna wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar.