WANANCHI WAIOMBA THBUB KUENDELEA KUTOA ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA MAENEO YA VIJIJI.
                            
                                 03 Jul, 2025
                            
                                
                             
                                
Wananchi  wameiomba Tume ya Haki za Binadamu  na Utawala Bora Kutoa elimu ya haki za binadamu  na utawala bora katika maeneo ya vijijini ili waweze kujua haki zao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Wananchi hao wamesema kuwa  watu wengi udhulumiwa haki zao  kutokana kuwa hawajui  mahala sahihi kupata haki zao pindiinapotokea imekiukwa.
"Unakutwa mtu amekamatwa bila kufuata utaratibu  tunaona sawa kwakua hatujui"amesema
Pia wananchi hao wameishukuru kwakufika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba ambapo imekua fursa kupata elimu hiyo

