ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Kongamano la Haki za Binadamu, Uzingatiaji wa Maadili na Kupiga Vita Vitendo vya Rushwa kwa Walimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

30 Nov, 2022

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kushirikiana na TAKUKURU imeandaa kongamano kwa walimu kwa ajili ya kuwajengea uelewa kuhusu haki za binadamu, uzingatiaji wa maadili katika utumishi wa umma na kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia na rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao.  Kongamano hili litafanyika tarehe 08 Disemba, 2022 katika Chuo Kikuu cha Dodoma ambalo litahusisha walimu wote wa chuo husika.