MFUMO WA PAMOJA KUWEZESHA TAASISI KUWASILIANA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka taasisi za umma ambazo hazijajiunga na mfumo wa pamoja unaowezesha mifumo mbalimbali ya serikali kuwasiliana na kubadilishana taarifa(Government Enterprise Services Bus-GoVesb) kuhakikisha kuwa zimejiunga katika mfumo huo kabla au ifikapo Juni 30, 2025
Hayo ameyasema Waziri Mkuu, Mhe.Majaaliwa Kassim Majaaliwa (Mb) wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika Viwanja vya Chinangali Park Dodoma Juni 23, 2025.
Mhe.Waziri amesema kuwa mfumo huu utasaidia kuboresha huduma zinazotolewa na serikali.
Sambamba na hilo, Mhe Majaaliwa amewataka watumishi kushiriki uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2025 kwa kuwa kuchagua ama kuchaguliwa ni haki ya msingi ya kikatiba.
"Tumieni haki hii"amesema Mhe.Majaaliwa
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yalifunguliwa 16,2025 na kuhitimishwa Juni23,2025.
Aidha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ni moja kati ya Taasisi 143 zilizoshiriki kutoa huduma katika Maadhimisho hayo