ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YAIMARISHA HAKI YA KUISHI KWA KUPANDA MITI

23 Jun, 2025
THBUB YAIMARISHA HAKI YA KUISHI KWA KUPANDA MITI


Viongozi na Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) wameshiriki katika zoezi maalum la upandaji miti lililofanyika katika bustani ya Tume hiyo iliyopo Nkuhungu, jijini Dodoma kwa lengo la kuimalisha haki ya kuishi mazingira safi na salama Juni 20,2025. 

Akizungumza wakati wa tukio hilo Makamu Mwenyekiti THBUB Kamishna Mhe.Mohamed Khamis Khamad amesema kuwa Tume inafahamu changamoto mbali mbali zinazohusu mazingira hivyo zoezi hili ni katika kuendeleza juhudi za Serikali katika kutatua changamoto hizo.

“Upandaji miti si tu zoezi la kimazingira, bali ni hatua ya kuimarisha haki ya kila Mtanzania kuishi katika mazingira salama, jambo ambalo lina uhusiano wa moja kwa moja na afya, usalama na ustawi wa jamii,” amesema Mh.Hamad.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Salama Kata ya Nkuhungu Bw. Habas Mwijuki ameshukuru Tume kwa kusaidia kuhifadhi na kuboresha eneo hilo kwani miti hiyo imesaidia kupunguza upepo na Kupata eneo la kivuli kwa ajili ya kuvuli wakati wa jua.

Bw. Mwijuki amewataka wananchi kuhakikisha wanatunza vyema miti hiyo na kuhakikisha kila mwananchi anapanda miti katika mazingira yake ili kuendelea kuboresha mazingira yanayowazunguka.

Nae Balozi wa Mazingira mkoa wa Dodoma Bw. Julian Bruno amepongeza THBUB na  ameeleza kuwa Tume imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika kuhakikisha mazingira yanatunzwa na kuhakikisha uhai wa binadamu unaendelea kuwepo.