UTEUZI
17 Jan, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan amemteua Jaji (Mstaafu) Mathew Pauwa Mhina Mwaimu kuwa Mwenyekiti na Bw. Mohamed Khamis Hamadi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume za Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kipindi cha pili.
Aidha, Rais Samia amewateua Makamisha wa Tume kama ifutavyo;-
i. Bw. Thomas Paulo Masanja, kuwa Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora
ii. Bi. Amina Talib Ali, kuwa Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora
iii. Bw. Khatib Mwinyi Khatibu, kuwa Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora na
iv.Bw. Nyanda Josiah Shughuli, kuwa Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora
Uteuzi huu ni kuanzia tarehe 15 January, 2023.