VIJANA WAASWA KULINDA AMANI NCHINI

Akizungumza wakati wa kuadhimisha Siku ya Sheria Chuo Kikuu cha Dodoma iliyofanyika Aprili 25,2025 katika Ukumbi wa CIVE Auditorium ulipo chuoni hapo Kamishna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe.Amina Talib Ali amesema kuwa amani ni kitu kikubwa sana nchini kabla na baada ya uchaguzi tuhakikishe kuwa maandalizi yote ya uchaguzi yanafanyika kwa amani bila kuleta machafuko.
“ Ni wajibu kila mwananchi mmoja kuhakikisha kwamba tunakwenda kwenye uchaguzi kukiwa na amani’
Pia Mhe Amina amesema kuwa miongoni mwa haki zilizotaja katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni haki ya kutoa maoni ikiwemo haki hii ya kupiga kura
“ hivyo kila mmoja ajue kwamba anayo haki ya kupiga kura lakini hakikisha unafuata sheria, miongozo na taratibu zilizopo’ amesema Mhe.amina
Mhe.Amina ameupongeza Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma kwakuchagua Mada ya ”Nafasi ya Kliniki za Sheria za Vyuo Vikuu katika kuhakikisha Uchaguzi Huru,Haki na Uwazi Tanzania”mada hii imeenda sambamba ikiwa tunaelekea katika uchaguzi mkuu mwaka huu