ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Balozi wa Sweden nchini Tanzania atembelea THBUB.

06 May, 2023
Balozi wa Sweden nchini Tanzania atembelea THBUB.

 

BALOZI wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Macias leo (Mei 5, 2023) ametembelea Makao Makuu ya Ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) zilizopo eneo la Kilimani jijini Dodoma na kufanya mazungumzo na uongozi wa juu wa taasisi hiyo. Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Balozi aliongoza ujumbe wa watu watatu.

Mheshimiwa Charlotta Ozaki Macias na viongozi wa Tume walizungumza masuala mbalimbali, ikiwemo mashirikiano baina ya taasisi zao, masula ya haki za binadamu na biashara, uhuru wa vyombo vya habari, mabadiliko ya Sheria ya Ndoa na mambo mengine.