ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Elimu ziendelee kutolewa kwa Jamii ili kuepusha Vitendo vya Mauaji ya kikatili katika Jamii.

22 Feb, 2022
Elimu  ziendelee kutolewa kwa  Jamii  ili kuepusha Vitendo vya Mauaji ya kikatili katika Jamii.

Haki ya kuishini haki ya binadamu,Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na Sheriaya kanuni ya adhabu sura 16 imeliweka kosa la Mauajikama kosa ambalo adhabu yake ni kifokwa maana anayefanya kosa hilo anapaswa na yeye kupata adhabu ya kifo.

Hayo amesema Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Mstaafu Mhe. Mathew Mwaimu katika mahojiano maalum na MwananchiDigital yaliyofanyika Februari 19,2022 katika Ofisi za THBUB Makuu Jijini Dodoma.

Mhe Mwaimu amesema kuwa ipo haja ya jamii kufahamu kuwa kila binadamu ana haki ya kuishi kama ilivyoelezwa katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na si vyema binadamu kujichukulia sheria mkononi kwa kufanya mauaji.

“Binadamu ndio kiumbee pekee aliyepewa nafasi kubwa hapa duniani,hivyo jamii ithamini na kuheshimu utu wa Binadamu”alisema Mhe.Mwaimu

Aidha Mhe.Mwaimu aliongeza kusema kuwaTHBUB kushirikiana na AZAKI,Asasi za Kiraia na Mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kuendelea kutoa elimu kwa Wananchi kuhusu maana ya haki ya kuishi

‘Tunatoa elimu ya mara kwa mara kupitia Vyombo vya habari naimani wote tukiungana tunaweza kufanikiwa kupunguza au kumaliza changamoto ya mauaji’’alisema Mhe.Mwaimu

Kwa hatua nyingine Mhe. Mwaimu ametoa wito kwa jamii kutoa malezi bora kwa watoto ili wakue katika maadili yatakayo heshimu haki za binadamu .

‘kuna sabababu za mbalimbali zinazopelekea mtu kuuaikiwemo mtu kutokubaliana na maamuzi,tamaa yakua na vitu asivokuwa na uwezo navyo,wivu wa mapenzi,kulipiza visasi,wazazi waone namna yakulea watoto katika maadili mazuri ili kuwa na kizazi kilicho chema’’alisema Mhe Mwaimu

Mhe.Mwaimu ametoashukrani kwa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe.Samia Suluhu Hassani kwakuendelea kusimamia Haki za binadamu na Misingi ya Utawala Bora