ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI

07 Oct, 2025
THBUB KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI

 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora itaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kulinda haki za binadamu na utawala bora.

Kauli hiyo imetolewa  Septemba 23, 2025 na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Mhe.Mathew Mwaimu wakati akifungua mafunzo kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kondoa, Mkoa wa  Dodoma

Mhe.Mwaimu amesema kuwa  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imekuwa ikishirikiana na Jeshi la Polisi katika  utoaji wa  elimu juu ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

‘’ushirikiano huu pia tunaupata pindi THBUB inapotembelea vituo vya polisi na kuzungumza na maabusu’’ amesema Mhe.Mwaimu

Aidha, Mhe.Mwaimu ameongeza kuwa katika kipindi hiki cha mchakato wa uchaguzi,  THBUB imejikita katika utoaji wa elimu kuhusu haki za binadamu na wajibu wa jeshi la polisi katika uchaguzi Mkuu

“ lengo la elimu hii ni kukumbusha juu ya masuala ya haki za binadamu wakati wa utekelezaji wa majukumu katika  kipindi hiki cha uchaguzi” amesema Mhe. Mwaimu


Kwa upande wake Mratibu Mwandamizi wa Polisi Wilaya ya Kondoa,  Bw. Desdeli Rugimbana ametoa pongezi kwa  THBUB kwa  kutoa mafunzo  hayo kwa Askari Polisi na kusema kuwa yatasaidia kuwakumbusha kutekekeza majukumu kwa kuzingatia haki za binadam