HAKI SPORT KLABU YAANZA VIZURI SHIMIWI
                            
                                 29 Sep, 2023
                            
                                
                             
                                Timu ya Wanaume Haki Sports Club ya Kamba imepata ushindi wa pointi 3 mara baada ya kuivuta mara zote mbili timu ya Kamba ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo Kaptein wa timu ya Kamba ya Wanaume ya Haki Bw. Kilua Mtae amesema kuwa, ushindi huo umepatikana kutokana na kujipanga vizuri na mashindano hayo.
Mbali na mchezo huo, pia timu ya Kamba ya Wanawake Haki Sports wameendelea kufunga ulingo kwa kutoka sare na kugawana pointi na na timu ya Wizara ya Viwanda na Biashara.

