ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Jaji Mwaimu na Naibu Mkurugenzi DIHR wakutana kuzungumzia mashirikiano

09 Apr, 2022
Jaji Mwaimu na Naibu Mkurugenzi DIHR wakutana kuzungumzia mashirikiano

Na Fadhili Muganyizi

MWENYEKITI wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Mathew Mwaimu (Jaji mstaafu) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Haki za Binadamu ya nchini Denmark (Danish Institute for Human Rights – DIHR), Bi. Eva Grambye hivi karibuni wamekutana kuzungumzia masharikiano baina ya taasisi zao.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Ijumaa Aprili 8, 2022 hoteli ya Holiday Inn jijini Dar es Salaam viongozi hao pamoja na mambo mengine walizungumzia mashirikiano kwenye masuala ya haki za binadamu na biashara na mradi wa upatikanaji wa haki (Access to Justice Project).

Pia, walizungumzia mustakabali wa mradi uliofanyiwa marejeo (Revised National Human Rights Action Plan), hususan majukumu ya Tume kwenye mradi huo na namna ambavyo DIHR inaweza kuisaidia Tume.

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Bi. Mette Spandet