emblem

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu

Habari

Jamii,Wadau pazeni sauti kwa pamoja kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya Watoto


Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi.Mary Makondo ameitaka Jamii na Wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana katika kupinga ukatili dhidi yawatoto.

Hayo amesemaJuni 6,2022 wakati wa kampeni ya uzinduzi wa siku kumi za kupinga ukatili dhidi ya Watoto yaliyofanyika katika Ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Bi Makondo alisema kuwa kumekuwa na changamoto kubwa mtoto kupata mimba akiwa shuleni na kupelekea kukosa ujasiri wa kutoa ushaidi mahakamani na kupelekea watuhumiwa wa makosa kuachiwa huru.

‘Nitoewito kwa wazazi ,jamii na wadau wengine kuheshimu haki za watoto na kuwapatia ulinzi stahiki ili kuepusha vitendo vya ukatili’.alisema Bi.Makondo

Aidha Bi.Makondo alibainisha takwimu za jeshi la polisi Tanzania kwa kipindi cha Mwaka 2021 jumla ya matukio 11,499 ya ukatili dhidi ya watoto yalitolewa taarifa vituo mbalimbali vya Polisi.Mikoa iliyoongoza ilikua ni Arusha(808),Tanga(691),Shinyanga(505),Mwanza(500) na Mkoa wa polisi Ilala(489).ambapo makosa yalioongoza kwa idadi kubwa ni ubakaji(5,899),mimba kwa wanafunzi(1,677) na ulawiti(1,114).

“Serikali,wadau na jamii *kwa ujumla tuunge mkono kampeni hii ya kupinga Ukatili dhidi ya Watoto ili kuendelea kutetea haki na ulinzi kwa watoto katika Jamii’’Alisema Bi.Makondo

AwaliMakamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Mohamed Hamisi alisema kuwa hali ya ukatili kwa Watoto inatisha sana,kwani imefikia hatua ya mzazi wa kiume kumlawiiti mtoto wake wa miezi 6.

“hali hii inasikitisha sana kwa sasa hatuoni ni nani wakuaminika katika jamii ikiwa hadi mzazi analawiti mtoto”.alisema Mhe. Mohamed

Kwa upande wake Inspekta Christer Kayombo Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Dodomaa aliwasihii watoto wasiogope kutoa taarifa Dawati la polisi wanapotendewa ukatili na endapo watashindwa basi wawambie wazazi au mwalimu wanayemwamini.

Uzinduzi wa kampeni hiyo ulitanguliwa na maandamano yaliyoanzia Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma hadi Ofisi za Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora zilizopo mtaa wa Kilimani.Kauli Mbiu “Tuimarishe ulinzi wa mtoto:Tokomeza ukatili Dhidi yake,Jiandae kuhesabiwa’’.

Kampeni hiyo ya uzinduzini sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Duniani ambayo hufanyika Juni16 kila Mwaka msingi wake ikiwa ni kutetea haki za Mtoto kama ilivyoelekezwa na Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto wa Mwaka 1990,unaobainisha kuwa Mtoto ana haki ya kuishi,kulindwa,kuendelezwa,kushiriki na kutobaguliwa.