ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

KAMISHNA WA THBUB ANAYESHUGHULIKIA HAKI ZA MAKUNDI MAALUM NA VIONGOZI WA ASASI YA FOUNDATION FOR DISSABILITIES HOPE

26 Sep, 2023
KAMISHNA WA THBUB ANAYESHUGHULIKIA HAKI ZA MAKUNDI MAALUM NA VIONGOZI WA ASASI YA FOUNDATION FOR DISSABILITIES HOPE

Kamishna wa THBUB anayeshughulikia haki za makundi maalum Mhe. Amina Talib Ali  amekutana na kufanya  kikao na viongozi wa Asasi ya Kiraia ya Foundation for Dissabilities yenye ofisi zake jijini Dodoma.

Mhe.Amina kuwa  THBUB wamekuwa wakifanya kazi mbalimbali katika kulinda haki za watu wenye ulemavu kama vile kufanya tafiti na kutoa huduma mbalimbali kwa watu wenye ulemavu.

Walieleza kuwa wakati wakitekeleza majukumu yao, wamekuwa wakibaini changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu na kwamba zinahitaji nguvu ya pamoja katika kuzishughulikia.

Aidha katika kikao hicho Mhe.Amina aliwapongeza  Viongozi hao kwa kazi nzuri wanayofanya kwakusimamia  haki za binadamu hususani yan watu wenye ulemavu.

“Niwapongeze kwa kazi nzuri ,ninyi mfano wa kuigwa katika kutetea haki za wanyonge”Alisema Mhe.Amina

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Foundation for Disabilities Michael Salali alieleza  kuwa  Hope (FDH) ni shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia masuala ya utetezi kwa haki na usawa wa makundi ya watu wenye ulemavu, vijana na watoto. Taasisi hii ilisajiliwa rasmi mwaka 2019 na kupata Usajili wa Taifa chini ya Sheria Na. 00NGO/R/004.

Bw. Alibainisha lengo la kufika  Ofisi za Tume ikiwa ni Kujadili namna ya Asasi hii itakavyoshirikiana na THBUB katika kutekeleza masuala mbalimbali kuhusu haki za binadamu hususan haki za watu wenye ulemavu; na Kuhamasisha kuhusu huduma inayotolewa na Shirika ya kuwajengea uwezo wa matumizi ya lugha ya alama watumishi katika ofisi za Serikali zinazotoa huduma kwa wananchi.

“Lengo kuu kufika  Tume kuweka kushirikiano baina ya Taasisi yetu na Tume ili kuendelea kwa pamoja kutetea haki za watu wenye ulemavu”Bwa.Salali

Wengine waliohudhuria kikao hicho ni Mkurugenzi Msaidizi –Utafiti na Nyaraka Bi. Fides Shao , Afisa Sheria na Utawala Bw. Method Faustine na Afisa fedha Bw. Fadhili Said.